Ofisa Mwandamizi wa Maendeleo ya Jamii, Idara ya Kuondoa Umasikini katika Wizara ya Fedha, William Ghumpi akimpatia Kitabu cha Taarifa ya Utekelezaji wa Malengo ya Milenia 2014, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo. Wapili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Na Salma Ngiwilizi – Maelezo
SERIKALI imewataka watumishi wa umma nchini kuonyesha ubunifu na weledi katika utendaji kazi wa majukumu yao mbalimbali ili kuweza kukidhi matarajio ya wananchi.
Aidha imewasisitiza watumishi wa umma wanawake kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na ufanisi ili kuonyesha uwezo wao na uhodari katika kutekeleza majukumu yao.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma HAB Mkwizu wakati akifungua maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Celina Kombani yanatoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
Kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Utumishi wa Umma katika Bara la Afrika ni chachu ya kuwawezesha Wanawake kuongeza Ubunifu na Kuboresha utoaji wa Huduma kwa Umma”.
Serikali imetoa miongozo mbalimbali ya kisera inayokusudia kumpa mwanamke wa nchi hii fursa sawa ya kuchangia maendeleo ya nchi yetu.
Baadhi ya miongozo hiyo ni pamoja na Sera ya Maendeleo ya Jamii ya mwaka 1996, Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000, na mwongozo wa anuai za jamii mwaka 2010.
Alisema hadi sasa utekelezaji wa miongozo hii umeleta matokeo chanya ambapo nchi yetu inajivunia kufikia mafanikio kadhaa , ambayo ni pamoja kuongezeka kwa idadi hya wanawake katika ngazi za maamuzi Serikalini kutoka asilimia 26 mwaka 2005 na kufikia asilimia 34 mwaka 2014.
“Wale waliopata nafasi walizopewa au kupata kutokana na juhudi zao. Ujuzi au uzoefu wao wanazitendea haki kwa kusimamia vizuri wale walio chini yao na kutoa huduma bora iliyotukuka kwa wananchi,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa mafanikio mengine ni kujenga uwezo wa watumishi wanawake kupata sifa za ziada ,kuongeza ubunifu na kuboresha upatikanaji wa huduma na Serikali imekuwa ikitoa ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamili kwa wanawake katika Vyuo Vikuu vya hapa nchini.
Hivyo katika kipindi cha miaka 10 jumla ya watumishi wanawake 251 walipatiwa ufadhili na kuhitimu masomo yao katika shahada mbalimbali za uzamili.
Alitoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia,sekta binfasi na vyombo vya habari kuendelea kutoa mchnago katika kuhimarisha Utumishi wa Umma katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
BOT YAWATAHADHARISHA WANANCHI
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, akimpatia vipeperushi Meneja Uhusiano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Zalia Mbeo, wakati alipotembelea banda la wizara katika maonesho ya Wiki ya Utumishi, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo.

Meneja Uhusiano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Zalia Mbeo, akimpatia maelezo Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu, kuhusu kazi ya Benki Kuu, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo.
Meneja Uhusiano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Zalia Mbeo, akimpatia maelezo Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu, kuhusu sarafu ya sh. 500, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo.
Meneja Uhusiano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Zalia Mbeo, akimpatia maelezo Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu, kuhusu sarafu ya sh. 500, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Na Salma Ngwilizi – Maelezo

BENKI ya Tanzania(BOT) imewataadharisha wananchi kwamba sarafu ya sh. 500 haina madini ya aina yoyote na wala haiuzwi haiuzwi kama inavyoadaiwa na baadhi ya watu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Zalia Mbeo wakati akitoa ufafanuzi kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mwizu ambaye aliuliza kwamba kuna taarifa kuhusu sarafu hiyo kuuzwa mitaani.
Kaimu Katibu Mkuu huyo ambaye alifungua maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Celina Kombani.
“Watanzania wanatapeliwa sarafu hii haina thamani yoyote ni uzushi,” alisema Zalia.
Aliongeza wananchi wadanganywa na watu kuwa sarafu hiyo ikiyeyushwa ina madini ambayo yanaweza kuwapatia fedha nyingi wakati si kweli.
Maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yamefunguliwa rasmi leo Juni 16, mwaka huu na yanatarajia kumalizika Juni 23, mwaka huu.
Kauli mbiu ya mwaka huu “Utumishi wa Umma katika Bara la Afrika ni chachu ya kuwawezesha Wanawake kuongeza Ubunifu na Kuboresha utoaji wa Huduma kwa Umma”.

No comments:
Post a Comment