TANGAZO


Tuesday, June 16, 2015

Komredi Kinana, Nape waunguruma Wilayani Chato

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Chato,mkoani Geita,wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi cya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye,akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Chato, Mkoa wa Geita wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi cya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Komredi Kinana akikagua gwaride la Chipukizi wa CCM, alipowasili katika Kata ya Kasenga, wilayani Chato, alipoanza ziara katika Mkoa wa Geita, baada ya kumaliza ziara katika Mkoa wa Kagera jana.
Komredi Kinana akikata utepe kuzindua rasmi Ofisi ya CCM Kata ya Kazunguti, wilayani Chato.
Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Kazunguti, wilayani Chato.
Komredi Kinana akizindua mitambo ya kusukuma maji katika mjini Chato.
Komredi Kinana akikagua mitambo hiyo ya kusukuma maji
Komredi Kinana akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa kikundi cha ujasiriamali ya Kilimani baada ya kuzindua mitambo ya kusukuma maji mjini Chato.
Komredi Kinana akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Mama mkazi wa  Chato yaliyotekwa kwenye bomba wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wilayani Chato.
Komredi Kinana akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Mama mkazi wa  Chato yaliyotekwa kwenye bomba wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wilayani Chato.

No comments:

Post a Comment