Katibu Mkuu wa CCM, Abdurahman Kinana akisalimia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara alifanya katika mji mdogo wa Katoto, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika mkoa wa Geita, jana, Juni 19, 2015.
Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM uliofurika maelfu ya wananchi katika mji mdogo wa Katoro, katika mkoa wa Geita, jana, Juni 19, 2015.
Maelfu ya wananchi wakiwa wamefurika kila kona katika mkutanowa hadhara uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika mji mdogo wa Katoro, jana, Juni 19, 2015.
Mbunge wa jimbo la Busanda, Lorencia Bukwimba, akihutubia katika mkutano wa hadhara wa Kinana uliofanyika katika mji mdogo wa Katoro, Juni 19, 2015.
Katibu Mkuu wa CCM, akiongoza kulima barabara, katikaKijiji cha Nyan'kanga, akiwa katika ziara ya kukagua ilani ya CCM na uhai wa Chama katika jimbo la Bsanda mkoani Geita, jana Juni 19, 2015.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga ripu, nyumba ya mganga inayoendelea kujengwa katika Zahanati ya Kijiji cha Inyala, jimbo la Busanda mkoani Geita.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na wananchi katika mkutano mdogo wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Chikobe, jimbo a Busanda mkoani Geita, jana, Juni 19, 2015.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana a wananchi kwa bashasha, alipowasili katika kijiji cha Nyan'kanga, katika jimbo la Buanda mkoani Geita, jana, Juni 19, 2015.
Wananchi wakishangilia katika Mkutano wa hadhara aliofanya Katibu Mkuu wa CCM katika Kijiji cha Nyan'kanga, katika jimbo la Busanda mkoani Geita, jana, Juni 19, 2015.
Katibu Mkuu wa CCM, akizungumzia kero ya wananchi kukosa maeneo ya wachimbaji wadogo kukosa eneo la uchimbaji kutokana na eneohilo kukaliwa na serikali na mwekezaji kwa zaidi ya miaka mitano sasa bila shughuliyoyote katika Kijiji cha Nyarugusu, jimbo la Busanda mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Viti maalum Vicky Kamata, alipowasili katika Kijiji cha Nyan'kanga, jimbo la Busanda mkoan Geita, jana, Juni 19, 2015. (Picha zote na Bashir Nkoromo).
No comments:
Post a Comment