TANGAZO


Saturday, June 20, 2015

Wanawake wakatazwa kushabikia mechi Iran

Wahifidhana wapinga wanawake kushabikia mechi ya mpira wa wavu dhidi ya Marekani
Wanaharakati nchini Iran wamekasirishwa na hatua ya kuwazuia wanawake nchini humo kushabikia mechi ya mpira wa wavu ya wanawake dhidi ya Marekani licha ya hakikisho kuwa wangeruhusiwa.
Kumekuwa na ripoti kwamba shirikisho la michezo nchini humo lingeruhusu idadi ndogo ya wanawake kushabikia mechi hiyo ya ijumaa ambayo Iran ilishinda 3-0.
Lakini upinzani wa taifa hilo ulio na wahafidhina huenda ndio uliosababisha shirikisho hilo kutoruhusu hatua hiyo.
Tamaduni za taifa hilo la kiislamu zinawakataza wanawake kushiriki katika michezo ya kiume.
Hatahivyo katika miezi ya hivi karibuni ,serikali ya rais Hassan Rouhani ilio na msimamo wa kadri imeonekana kusikiza shiniko za wanaharakati na zile za mashirika ya michezo ya kimataifa kupunguza vikwazo.
Shahindokht Molaverdi,makamu wa rais wa maswala ya wanawake na yale ya familia aliwaambia maripota wiki iliopita kwamba wanawake wataruhusiwa kushabikia mechi ya mchezo wa mpira wa wavu upande wa wanawake dhidi ya Marekani.
Na mapema wiki hii,shirikisho la mchezo wa mpira wa wavu FIVB lilisema limehakikishiwa kwamba wanawake wataruhusiwa kushabikia mechi hiyo katika uwanja wa michezo Tehran Azadi.

No comments:

Post a Comment