TANGAZO


Wednesday, June 24, 2015

Hitimisho la Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akipatiwa maelezo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, wakati alipotembelea banda la wizara hiyo, katika siku ya mwisho ya maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akiweka saini kitabu cha wageni kwenye banda la Wizara ya Nishati na Madini, alipotembelea banda la hilo, katika siku ya mwisho ya maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.



Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akimkabidhi kikombe cha ushindi wa Pili kwa Taasisi zenye mifumo bora ya Utendaji, Kaimu Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Gaudensia Simwanza, wakati wa ufungaji wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana. 










Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika ufungaji wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.


Waimbaji wa Msondo Band, wakizirudi ngoma, wakati wa ufungaji wa Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.

Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wakiwa katika picha ya pamoja na Tuzo zao  walizojishindia katika nyanja mbalimbali mara baada ya kukabidhiwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati wa kilele cha maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.


Na Eleuteri Mangi –MAELEZO
MAONESHO ya wiki ya Utumishi wa Umma yamefikia kilele jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, ambapo shughuli mbalimbali zilifanyika kwa juma zima ikiwemo kuelimsha wananchi juu ya kazi zinazofanywa na Serikali kupitia Wizara zake, Taasisi na Mashirika ya Umma. 

Katika kuhitimisha maonesho hayo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Musa Assad ameshauri Serikali kuwa ni vema ikahakikishe inatoa ajira katika nafasi mbalimbali hasa nafasi za juu kwa waombaji wenye vigezo vinavyohitajika ili kuepuka upendeleo na maslahi binafsi katika ofisi za Serikali. 

Ili kuhakikisha ajira zinatolewa kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa, Prof. Assad ameishauri Serikali kuzingatia vigezo vilivyowekwa wakati wa kuajiri watumishi katika nafasi mbalimbali za uongozi ili utendaji kazi uwe wa uadilifu na wenye tija usiokuwa na maslahi binafsi.

Prof. Assad alitoa ushauri huo alipokuwa akiongea katika kipindi maalumu cha maonesho ya wiki ya utumishi wa Umma kilichorushwa televisheni ya taifa (TBC1).

Aidha, kwa kuzingatia umuhimu wa vyombo vya habari nchini, Prof. Assad amevishauri vyombo hivyo kuzingatia maadili ya taaluma hiyo kwa weledi katika kutimiza wajibu na majukumu yao ya kuhabarisha umma.

Monyesho hayo yalifungwa rasmi jana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alli Hssan Mwinyi ambapo viongozi mbalimbali wametembelea maonesho hayo akiwemo katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ambaye amewashauri wananchi kujenga tabia ya kutembelea maonesho mbalimbali nchini.

Baadhi ya Wizara na Taasisi za Serikali zilizoshiriki maonyesho hayo ni pamoja na Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Wakala wa Vipimo (TMA), Mamlaka za Usafiri wa Anga (TCAA), Bohari ya Dawa (MSD), Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (RITA) na Wakala ya Serikali Mtandao (eGA).

No comments:

Post a Comment