TANGAZO


Saturday, May 9, 2015

Simba yashika nafasi ya Tatu Ligi Kuu ya Vodacom, yaichapa JKT Ruvu mabao 2-1, wachezaji wakabidhiwa medali zao Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Askari wakiangalia mpira huku sehemu kubwa ya Uwanja wa Taifa, ikiwa haina watazamaji, wakati wa mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na JKT Ruvu. Simba ilishinda mabao 2-1 katika mchezo huo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Nurdin Mohamed wa Ruvu JKT , akiangalia wapi kwa kupeleka mpira, wakati wa mchezo dhidi ya Simba, leo Uwanja wa Taifa.
Nurdin Mohamed wa Ruvu JKT , akimtoka Issa Abdallah wa Simba, leo Uwanja wa Taifa. 
Issa Abdallah wa Simba akikimbia na mpira wakati wa mchezo huo leo, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. 
Emmanuel Okwi wa Simba na Nurdin Mohamed wa Ruvu JKT wakiwania mpira  wakati wa mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba ilishinda mabao 2-1 na hivyo kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo.
Emmanuel Okwi wa Simba na Nurdin Mohamed wa Ruvu JKT wakiwania mpira  wakati wa mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba ilishinda mabao 2-1 na hivyo kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo. 
Nurdin Mohamed wa Ruvu JKT, akitafuta mbinu ya kumpita Emmanuel Okwi wa Simba, wakati wa mchezo huo.
 Nurdin Mohamed wa Ruvu JKT, akimtoka Emmanuel Okwi wa Simba, wakati wa mchezo huo.
Nurdin Mohamed wa Ruvu JKT, akiupiga mpira huku akifuatwa na Okwi wa Simba.
Emmanuel Okwi wa Simba, akiupiga mpira huku  akifuatwa na Nurdin Mohamed wa Ruvu JKT, wakati wa mchezo huo.
Mchezaji Jonas Mkude wa Simba, akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Jaffary Kissoky wa JKT Ruvu wakati wa mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba ilishinda mabao 2-1.
Jonas Mkude wa Simba, akiwania mpira na Jaffary Kissoky wa JKT Ruvu wakati wa mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba ilishinda mabao 2-1. 
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo dhidi ya JKT Ruvu leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba ilishinda mabao 2-1.
Nurdin Mohamed wa Ruvu JKT, akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Jonas Mkude (kulia) na Issa Abdallah (17), wote wa Simba.
Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi Mkoa wa Dar es Salaam, Salim Chama akimvisha medali Emmanuel Okwi wa Simba baada ya timu hiyo kuibuka washindi wa Tatu kwa kuifunga JKT Ruvu mabao 2-1, katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Idrissa Rashid 'Baba Ubaya' wa timu hiyo. 

Juu na Chini: Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi Taifa (FRAT), Salim Chama akiwavalisha medali wachezaji na viongozi wa Simba mara baada ya timu hiyo kuibuka mshindi wa Tatu kwa kuifunga JKT Ruvu mabao 2-1, katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
 Abdallah Seseme akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi Taifa (FRAT), Salim Chama, wakati wa kuvalishwa medali.
Ivo Mapunda akikabidhiwa medali yake. 
Msemaji wa Simba, Haji Manara, akivishwa medali.

No comments:

Post a Comment