Mtayarishaji wa filamu na mwimbaji wa siku nyingi
Jennifer Mgendi anakusudia kuachia filamu yake ya “Nipo Studio” mapema wiki
hii. Akiongea na blogu hii Jennifer amesema filamu hiyo imekamilika kwa kila
kitu na itaingia sokoni wiki hii ikiwa imewashirikisha wasanii mbalimbali
akiwamo shosti wake wa siku nyingi Bahati Bukuku, Bibi Esta, Hassan Mbangwa,
Gwamaka Kametta na wengine wengi.
Jennifer amesema filamu hii inazungumzia changamoto
mbalimbali anazokutana nazo Bibi Esta pale anapokuwa na ndoto ya kuwa mwimbaji
huku umri na kipato vikiwa kikwazo kwake.
Wakati huo huo Jennifer amesema maandalizi ya tamasha lake la
uzinduzi wa video ya Wema ni akiba yanaendelea vizuri na tamasha hilo
litafanyika kama ilivyopangwa tarehe 28 Juni katika kanisa la DCT Tabata Shule
huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies
of God , Dr. Barnabas Mtokambali.
No comments:
Post a Comment