Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya Marehemu John Nyerere, mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tarehe 9.5.2015. Shughuli ya kuaga mwili wa marehemu John ilifanyika nyumbani kwa Mwalimu Nyerere huko Msasani tarehe 11.5.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume (wa nne kutoka kushoto) pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro wamesimama mbele ya jeneza wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu John Nyerere iliyofanyika Msasani tarehe 11.5.2015. Mwili wa Marehemu John unatarajiwa kusafirishwa tarehe 12.5.2015 kwenda Butiama kwa mazishi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Mama Maria Nyerere mara baada ya shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu John Nyerere huko Msasani. Marehemu John anatarajiwa kuzikwa Jumatano tarehe 13.5.2015 katika kijiji cha Butiama, Mkoani Mara. (Picha zote na John Lukuwi)
No comments:
Post a Comment