Mwanahabari Deogratias Mongela wa Kampuni ya Global Publishers Ltd.
Bibi Harusi, Elizabeth Sanga.
Deogratias Mongela akiwa na mke wake Elizabeth Sanga wakati wa hafla ya ndoa yao iliyofanyika Hoteli ya Atriums iliyopo Sinza Afrikasana baada ya kufunga ndoa Katika Kanisa la Katoliki, Parokia ya Mbezi Luis Dar es Salaam jana.
Maharusi hao (katikati) wakiwa na wapambe wao kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Cobson Nzige na mke wake Subira Nzige (kulia), 'hakika wamependeza si mnawaona'.
Mama mzazi wa Bwana harusi, Asia Kapori akiwahasa
maharusi hao.
Mjomba wa Bwana harusi, Karim Mtambo na pia akiwahasa maharusi hao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo akimpongeza bwana harusi Deogratias Momgela baada ya kuoa. Wengine ni wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo (katikati), akijumuika na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Mhariri, Amrani Kaima na Oscar Ndauka wa kampuni hiyo.
Mama mzazi wa Deogratias, Asia Kapori akiwasalimia wageni mbalimbali kwenye sherehe hiyo.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakipata kinywaji kwenye hafla hiyo.
Mwanahabari Kulwa Mwaibale wa kampuni hiyo akiteta jambo
na Bwanaharusi.
Maharusi hao wakiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Maharusi na wapambe wao wakiserebuka pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani), (Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)
No comments:
Post a Comment