Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana Viongozi wa Chama CCM wakati alipowasili Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba aliposhiriki katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi wakati alipowasili katika Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo.
Maandamano ya wafanyakazi wa Taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi Kisiwani Pemba yakiingia katika uwanja wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Wilaya ya Chakechake leo wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani na kupokelewa na mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein(katikati) akipunga mkono kupokea maandamano ya wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na Binafsi kisiwani Pemba wakati akilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Uwanja wa Kiwanja Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) akipunga mkono kupokea maandamano ya wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na Binafsi kisiwani Pemba wakati wa Kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Uwanja wa Kiwanja Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba.
Wafanyakazi wa Wizara ya Afya Kisiwani Pemba wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akipokea maandamano ya wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na Binafsi wakati wa Kilele cha sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Uwanja wa Kiwanja Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba.
Wafanyakazi wa ZSTC Pemba wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akipokea maandamano ya wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na Binafsi wakati wa Kilele cha sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Uwanja wa Kiwanja Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba.
Viongozi mbali mbali na wafanyakazi wakiwa katika ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba wakati wa sherehe za Siku ya Kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) pamopja na Viongozi wengine wakinyanyua mikono juu wakati wakiimba wimbo maalum wa Mshikamano (Solidarity Forever) wakati wa kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani sherehe zilizofanyika leo Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Wilaya ya Chake chake Pemba.
Viongozi na Wafanyakazi Mbali mbali wakishikamana kunyanyua mikono juu wakiimba kwa pamoja na kuimba wimbo maalum wa Mshikamano (Solidarity Forever) wakati wa kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani sherehe zilizofanyika leo Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Wilaya ya Chake chake Pemba.
Wafanyakazi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akiwahutubia wafanyakazi wa taasisi mbali mbali za Serikali na Taasisi Binafsi wakati wa Kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Wafanyakazi na Wananchi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiwahutubia wafanyakazi wa taasisi mbali mbali za Serikali na Taasisi Binafsi katika sherehe za Kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi Bi Khadija Hamadi Abdalla wa Ofisi ya Rais (MBLM) ZUPHE Cheti na Fedha tasilim Shilingi Laki Tano katika sherehe za Kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi Bw. Abdalla Haji Abdalla wa Ofisi ya Rais (MBLM) ZUPHE Cheti na Fedha tasilim Shilingi Laki Tano katika sherehe za Kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi Bw. Seif Suleiman Kassim wa shirika la ZSTC tawi la TUICO-Z Cheti na Fedha tasilim Shilingi Laki Tano katika sherehe za Kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi Bw. Suleiman Hamadi Suleiman wa shirika la Bandari tawi la COTWU-Z Cheti na Fedha tasilim Shilingi Laki Tano katika sherehe za Kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi Bi Mwanahamis Kombo Ali wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais ZUPHE Cheti na Fedha tasilim Shilingi Laki Tano katika sherehe za Kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi Kikombe Nahodha wa Timu ya Bandari Ali Makame Akida baada ya timu yake kuifunga Timu ya Ikulu kwa mabao 2-1katika mchezo wa fainali kombe la Mei Day kikombe hicho kilikabidhiwa katika sherehe za Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo Viwanja vya kiwanda cha makonyo Wawi Wilaya ya Chakechake Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akiwahutubia wafanyakazi wa taasisi mbali mbali za Serikali na Taasisi Binafsi wakati wa sherehe za Kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Wafanyakazi waliochaguliwa kuwa wafanyakazi Bora wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akiwahutubia wafanyakazi wa taasisi mbali mbali za Serikali na Taasisi Binafsi wakati wa sherehe za Kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi bora wa taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi baada ya kuwakabidhi vyeti na fedha taslim katika sherehe za Kilele cha Siku ya wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.(Picha zote na Ikulu)
Na Said Ameir, Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewahakikishia watumishi wa umma kuwa Serikali itawalipa, mapema kwenye mwaka wa fedha unaoanza Julai 2015/2016, malimbikizo yao yote ya madai yanayotokana na kasoro zilizojitokeza wakati wa marekebisho ya mishahara na posho.
Akizungumza na wafanyakzi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani leo yaliyofanyika katika viwanja vya Kiwanda cha Mkonyo kilichoko Wawi wilaya ya Chakechake Pemba, Dk. Shein amewahakikishia watumishi hao kuwa Serikali inazifanyia kazi kasoro hizo na kuwahakikisha kuwa hakuna mtumishi atakayepoteza haki yake.
“Serikali inaendelea kuyahakiki malimbikizo hayo na tayari tumeshafanya uamuzi wa kuyalipa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016”alisisitiza Mheshimiwa Rais.
Sambamba na kuwahakikishia malipo hayo, Dk. Shein alibainisha kuwa hatua zote zinazochukuliwa na Serikali kuimarisha hali ya wafanyakazi lengo lake ni kulifanya suala la kuwapatia maslahi bora watumishi wa umma liwe ni suala endelevu kadri uchumi unavyoimarika.
Miongoni mwa hatua hizo ambazo amezitaka kuwa ni miongoni mwa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Saba katika kuimarisha utumishi wa umma ni kupitisha sheria mbalimbali zikiwemo Sheria Na. 2 ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2011.
Aidha alieleza kuwa kanuni 12 za Sheria za Kazi zimetungwa katika kipindi hiki na kuanza kutumika miongoni mwao ni za Sheria ya Ajira Namba 11, Sheria ya Mahusiano Kazini Namba. 1, zote za mwaka 2015 na Kanuni za mwaka 2014 za Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya mwaka 2011.
Katika mnasaba huo ametoa wito kwa watumishi na waajiri kusoma vyema na kufahamu Sheria ya Utumishi wa Umma ya Mwaka 2011 kwa kuwa ndio msingi wa mambo yote yanayohusu sheria, maslahi, makosa na adhabu zake.
Dk.Shein aliwaeleza wafanyakazi hao kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha Sera ya Usalala Kazini ili kuweka mfumo mzuri wa afya katika maeneo ya kazi kwa lengo la kuwakinga wafanayakazi na ajali na majanga mengine katika sehemu za kazi.
Kwa hivyo aliwataka watumishi wote nchini kuendelea kufanyakazi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za kazi zinavyoelekeza na kusisitiza kuwa ni lazima katika utendaji wao kuhakikisha kuwa wanatenda haki na kuwaheshimu wananchi kwa kuwa Serikali yote akiwemo yeye mwenyewe Mheshimiwa Rais wanawajibika kwa wananchi.
Katika hotuba yake hiyo Dk. Shein aliipongeza Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma kwa kazi nzuri inayofanya kuratibu na kuweka uhusiano mzuri kati ya Serikali, wafanyakazi na kusimamia ipasavyo Sera na Sheria mbalimbali zinazohusu kazi na ajira.
Kwa hivyo aliwahakikishia kuwa Serikali anayoiongoza inazingatia sana umuhimu wa uhusiano huo na siku zote itakuwa tayari kushirikiana nao kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wafanyakazi wote Unguja na Pemba.
Katika hatua nyingine Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amewasihi wafanyakazi na wananchi kwa jumla kuhakikisha kuwa wanashiriki vyema katika uchaguzi mkuu ujao huku wakizingatia kuendeleza mafanikio ya kuimarisha amani, umoja na mshikamano.
“Halitakuwa jambo jema utaratibu huu wa kidemokrasia ukawa ni chanzo cha kuvuruga amani, umoja na mshikamano” Dk. Shein alisisitiza na kuongeza kuwa aliyedhamiria kutenda lake aseme na nafsi yake kwanza kabla hajafanya hivyo.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman alieleza kuwa katika kukuza uelewa wa jamii kuhusu sheria za kazi, sheria za kazi za Zanzibar zimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani(ILO) imeziweka sheria hizo katika lugha nyepesi.
Waziri Haroun alibainisha kuwa Wizara yake inaendelea na zoezi la uwekaji wa taarifa za watumishi wa umma katika mfumo wa kieletroniki hatua ambayo itasaidia katika kuimarishaji wa kutunza kumbukumbu za taarifa zao na kulinda haki zao wakiwa kazini na baada ya kustaafu.
Aidha Wizara yake alisema imefanikiwa kupunguza migogoro ya kazi kutoka 179 mwaka 2012/2013 hadi migogoro 102 mwaka 2013/2014.
Awali akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi Zanzibar-ZATUC Bwana Khamis Mwinyi Mohamed alimpongeza Mheshimiwa Rais kwa utayari wake wakati wowote kushirikiana na Shirikisho hilo kitendo ambacho kimezidi kujenga mahusiano mazuri kati ya Shirikisho na Serikali.
Aliipongeza Serikali kwa kutoa fursa kwa wafanyakzi kushiriki katika michakato mbalimbali ya masuala ya kitaifa hivyo kuwafanya kuwa sehemu ya maamuzi na matokeo yatokanayo na michakato hiyo.
Katibu Mkuu huyo aliiomba serikali kuangalia upya kodi zinazotozwa wafanyakazi katika mishahara pamoja na malipo ya viinua mgongo na pensheni.
Nae Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Zanzibar (ZANEMA) Bwana Salah Salim Salah alisisifu kuzidi kuimarika kwa mahusiano kati ya waajiri na wafanyakazi jambo ambalo limerahisisha utatuzi wa migogoro baina ya pande mbili hizo.
Hali hiyo imewezesha kuwepo na mawasiliano na mashauriano ya mara kwa mara kati ya pande hizo na kuondokana na yale yaliyotokea zaid ya miaka 126 huko nchini Marekani ambako wafanyakazi walipodai haki zao walikumbana na kadhia na vurugu zilizosababish baadhi yao kupoteza maisha.
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa mwaka huu ni mwaka muhimu kwa wajiri na wafanyakazi kama walivyo wananch iwenginek kutokana na nchi yetu kuelekea Uchaguzi Mkuu kwa kuhakikisha uchaguzi huo haiwi chanzo cha vurugu ambazo zinaweza kuharibu nchi na uchumi wake.
Katika maadhmisho hayo Mheshimiwa Rais alikabidhi zawadi mbalimbali kwa watumishi bora kutoka ofisi na taasiii mbalimbali za umma.
No comments:
Post a Comment