TANGAZO


Friday, May 1, 2015

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Hafsa Mtasiwa awataka wananchi kuisoma na kuilewa Katiba inayopendekezwa

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Hafsa Mtasiwa (kushoto), akiwa kazini.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Hafsa Mtasiwa (kushoto), akiwa kazini.


Na Fredy Mgunda, Iringa
WANANCHI wa mkoa wa tanga wilaya ya korogwe wametakiwa kuisoma na kuilewa katiba inapendekezwa ili waweze kuipigia kura.

Akizungumza na blog hii Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Hafsa Mtasiwa, amewataka wananchi wa wilaya hiyo, kusoma na kuijadili katiba hiyo na kutosikiliza maneno kutoka kwa watu.

Aidha Mtasiwa amesisitiza kuwa Tanzania bado tunakatiba yetu na tupo kwenye mchakato wa kupata katiba mpya hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini na maneno wanayo ambiwa na watu wengine.

“Katiba inayopendekezwa imeandikwa na binadamu wa kawaida kama ilivyokuwa hapo awari katika katiba ambayo inatumika hadi sasa lakini inapaswa kuangalia kuna mambo gani mapya ambayo yameandikwa kwenye katiba inayopendekezwa na imebeba mambo gani muhimu katika maendeleo ya Tanzania yetu”.alisema mtasiwa

Lakini Mtasiwa ameendelea kuwataka watanzania kwa ujumla kuendelea kuidhamini amani tulivyo nayo kwa sasa na tusiwafuate wananchi wengi wenye lengo la kuvuruga amani yetu kwa maslai yao binafsi hivyo watanzania msidaganyike kwa maneno yao.

Mtasiwa amewaomba wazazi wote kuwapa elimu ya kutosha watoto wao juu ya kutunza amani na kuacha tabia ya kushabikia maneno ya uchochezi yenye lengo la kuvuga amani yetu.

Wakati huohuo Mtasiwa amewataka wananchi wa wilaya hiyo kujua umuhimu wa kutumia bima na wajitokeze kuchangia katika mifuko ya bima.

Bima ya Afya inafaida kubwa sana katika maisha yako hivyo lazima wananchi watambue umuhimu wa kuchangia bima kwa kuwa serikali imepanga kuwachangia wananchi kwa kiasi kile ambacho wamekichanga kwa mfano wananchi wakichanga milioni 100 na serikali itatoa milioni 100 kwa lengo la kuboresha sekta ya afya, alisema Mtasiwa.

No comments:

Post a Comment