UNFPA, UNICEF, Shirikisho la Kimataifa la Wakunga na Shirikisho la Kimataifa la Magonjwa ya Wanawake na Uzazi.
Wito kwa wafanyakazi wa afya duniani kote ili kuhamasisha kukomesha ukeketaji
Kwa
mwaka 2015, ujumbe wa kimataifa wa siku ya kupinga ukeketaji umewalenga
wahudumu wa afya; “Uhamasishaji na ushirikishwaji wa wafanyakazi wa
Afya ili kuharakisha kutokomeza ukeketaji.
Na hii ni kwa sababu
asilimia 34 ya ukeketaji duniani hufanywa na wahudumu wa afya.
Pamoja na ujumbe huu mahsusi kwa wahudumu wa afya, wadau wengine wote unawahusu.
Ujumbe unasema hivi:
Ukeketaji
wa wasichana na wanawake unakiuka haki za binadamu na unadhoofisha afya
na ustawi wa wasichana takriban milioni 3 kila mwaka. Zaidi ya
wasichana na wanawake milioni 130 katika nchi 29 barani Afrika na
Mashariki ya Kati ambapo hadi leo hii vitendo hivi vimekithiri
wamekwisha fanyiwa aina fulani ya ukeketaji - na athari kwa maisha yao
ni kubwa sana.
Duniani
kote, tunashuhudia kuongezeka kwa utayari wa jamii na serikali ili
kuondokana na vitendo vya ukeketaji - lakini hii haitoshi kwani jitihada
zaidi zinahitajika.
Leo, tunapoadhimisha Siku ya Kimataifa ya kukomesha
ukeketaji dhidi ya watoto wa kike, tunatoa wito kwa wafanyakazi wote wa
afya – kuanzia wakunga, wauguzi madaktari wa magonjwa ya wanawake na
watu wote katika sekta ya Afya kutoa hamasa dhidi ya kukomesha vitendo
vya ukeketaji wa watoto wa kike.
Mchango
wa wafanyakazi wa sekta afya katika jitihada za kimataifa za kukomesha
ukeketaji dhidi ya watoto wa kike ni muhimu sana kwani wana uelewa mpana
wa mienendo na desturi ya kijamii katika jumuiya wanazozihudumia. Hivyo
wafanyakazi wa afya wanaweza kuharakisha kupungua kwa kasi kwa vitendo
vya ukeketaji kwani watu wanaowahudumia wana imani kubwa dhidi yao.
Wafanyakazi
wa afya pia wana uelewa wa kina juu ya madhara yanayotokana na vitendo
vya ukeketaji kwani wanashuhudia madhara katika njia ya mkojo, njia ya
hedhi, maambukizi katika via vya uzazi ikiwa ni pamoja na kutoka damu
nyingi na hatimae vifo, pia hushuhudia athari za kisaikolojia dhidi ya
wale waliofanyiwa vitendo vya ukeketaji hali ambayo ni ya kudumu katika
maisha yao.
Wafanyakazi wa afya pia wapo katika nafasi nzuri ya kuongoza jitihada za kupinga mienendo mibaya inayoibuka katika nchi nyingi.
Katika
baadhi nchi ukeketaji unafanywa na wahudumu wa afya, mathalan takriban
msichana mmoja kati ya watano wamekeketwa na watoa huduma waliopatiwa
mafunzo, na katika nchi zingine idadi hii inaongezeka inafikia kati ya
wasichana watatu hadi wanne.
Ukeketaji
ni kinyume cha sheria katika nchi nyingi, Tanzania ikiwemo chini ya
sheria ya masuala ya kujamiiana 1998, na watoa huduma za afya ambao
wanafanya vitendo hivyo katika maeneo haya wana vunja sheria.
Ifahamike
kuwa katika nchi zote, aidha sheria zao ziwe zinaruhusu au haziruhusu
vitendo vya ukeketaji ni kukiuka haki za msingi za wanawake na
wasichana.
Wataalamu
wa afya hususan wale walio katika zahanati na vituo vya afya mara
nyingi wanaweza kuwa na shinikizo kubwa la kufanya ukeketaji.
Lakini
endapo watahamasishwa kupinga shinikizo hilo, wanaweza kuwa sehemu ya
ufumbuzi.
Hivyo,
kwanza kabisa, tunatoa wito kwa wafanyakazi wote wa afya kama wapo
wanaoshiriki vitendo vya ukeketaji kuachana na vitendo hivyo na kutumia
ushawishi walionao katika jamii wanazofanyia kazi na kuhamasisha wenzao
katika jamii zingine kukomesha vitendo vya ukeketaji katika maeneo yote.
Pia tunatoa wito kwa wafanyakazi wote wa afya kulinda afya ya uzazi na
ujinsia ya wasichana wote ambao tayari wamekeketwa.
Tunajua
kwamba wafanyakazi wa afya hawawezi kufanya hivyo peke yao.
Mashirika kama UNFPA, na UNICEF, kupitia mpango wetu wa Pamoja wa kukomesha ukeketaji, pamoja na Shirikisho la kimataifa la Wakunga, na Shirikisho la Kimataifa la magonjwa ya wanawake na uzazi, tuko tayari na tunayo nia ya kusaidia jitihada za kuwapatia wafanyakazi wa afya ujuzi na taarifa yoyote itakayohitajika ili kuongeza kasi katika kukomesha ukeketaji na pia kutoa tiba dhidi ya madhara yaliyotokana na ukeketaji.
Mashirika kama UNFPA, na UNICEF, kupitia mpango wetu wa Pamoja wa kukomesha ukeketaji, pamoja na Shirikisho la kimataifa la Wakunga, na Shirikisho la Kimataifa la magonjwa ya wanawake na uzazi, tuko tayari na tunayo nia ya kusaidia jitihada za kuwapatia wafanyakazi wa afya ujuzi na taarifa yoyote itakayohitajika ili kuongeza kasi katika kukomesha ukeketaji na pia kutoa tiba dhidi ya madhara yaliyotokana na ukeketaji.
Kanuni
za kijamii, hususan katika jamii ambazo zina mshikamano na umoja huwa
zina nguvu kubwa juu ya maisha na mienendo ya jamii husika. Lakini
kanuni hizi zinaweza kubadilika endapo watu wataamua kufanya hivyo. Pia
endapo wafanyakazi wa afya, viongozi, wataalam, na, zaidi ya yote,
wasichana na familia kwa ujumla, watakemea na kuchukua hatua dhidi ya
mienendo mibaya.
Katika
Siku ya Kimataifa ya kukomesha ukeketaji, Tushikamane kupinga ukeketaji
kwani Afya, Haki na Ustawi wa mamilioni ya wasichana unategemea umoja
wetu.
No comments:
Post a Comment