Morocco imepigwa marufuku kushiriki katika michuano miwili ya kombe la Afrika baada ya kushindwa kuandaa michuano ya mwaka huu.
Shirikisho la soka nchini humo pia limepigwa faini ya dola millioni moja na kuagizwa kulipa yuro millioni 8 kama faini ya uharibifu.
Morocco ilionyesha wasiwasi wake kuhusu maandalizi ya dimba hilo kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola barani Afrika.
Waliomba michuano hiyo kuahirishwa hadi mwaka 2016.lakini shirikisho la soka barani Afrika CAF likakataa ombi hilo.
Equitorial Guinea walichukua mahala pa Morrocco kuandaa michunao hiyo huku Morocco ikipigwa marufuku kushiriki.
CAF pia iliipiga marufuku dola laki moja baada ya mashabiki wake kuzua ghasia katika mechi ya nusu fainali kati yake na Ghana.
No comments:
Post a Comment