Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi Daniela Schadt (mwenye nguo nyekundu) akisalimiana na
Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga mara baada ya kuwasili katika ofisi
za Shirika hilo zilizopo Tengeru jijini Arusha alipoenda kuzindua mradi wa
BEYOND 2015 hivi karibuni.
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi Daniela Schadt (mwenye nguo nyekundu) akisikiliza maelezo
mafupi kuhusu Shirika lisilo la Kiserikali la DSW Tanzania kutoka kwa
Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Peter Owaga mara baada ya kuwasili katika ofisi
za Shirika hilo zilizopo Tengeru jijini Arusha juzi. Wa mwisho kushoto ni Mkuwa
Wialaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe Munasa.
Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa BEYOND 2015 juzi jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Mke wa Rais wa Shirikisho la Ujerumani Bibi Daniela Schadt, Mke wa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bibi Wenday Marshall – Kochanke na Mratibu wa Programu za Vijana kutoka Wizara ya Afya, na Ustawi wa Jamii Dkt. Elizabeth Mapella. BEYOND 2015 ni mradi uliolenga kuongeza hamasa na ushawishi kwa wadau wa maendeleo kutoa kipaumbele kwa vijana husasni katika Elimu, Afya ya uzazi na Ajira.
Baadhi ya washiriki wa
hafla ya uzinduzi wa mradi wa BEYOND 2015 wakimsikiliza Mkurugenzi wa DSW
Tanzania Bw. Peter Owaga (hayupo pichani).
Mkewa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi Daniela Schadt(mwenye nguo nyekundu)
akisikiliza maelezo kuhusu mradi wa BEYOND 2015 kutoka kwa Mratibu wa mradi huo
Bi. Esther Mwanjesa (kushoto) kabla ya kuzindua rasmi mradi huo juzi jijini
Arusha. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga na
kushoto kwa Mke wa Rais wa Ujerumani ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe
Munasa.
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi Daniela Schadt akifuarahi mara baada
ya kukata utepe na kuzindua rasmi mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini
Arusha.Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa DSW Tanzania ambao ndiyo watekelezaji wa
mradi huu Bw. Peter Owaga. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe
Munasa (nyuma ya Mke wa Rais wa Ujerumani) na Mratibu wa Mradi huo Bi. Ester
Mwanjesa aliyeshika kitabu.
Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya
Ujerumani Bibi Daniela Schadt akiteta jambo na Mkurugenzia wa DSW
Tanzania (katikati) pamoja na Mratibu wa Mradi wa BEYOND 2015 Bi. Esther
Mwanjesa mara baada ya kuzindua mradi huo juzi jijini Arusha.
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bi. Daniela Schadt akipokea zawadi ya
Kimasai kutoka kwa Mwanamke mjasiriamali Bibi Salome Samwel wakati
alipotembelea maonyesho ya biaadha zao katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa
mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini Arusha.
Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani
Bi. Daniela Schadt akivaa heleni alizopewa kama zawadi kutoka kwa Mwanamke wa
mjasiriamali Bibi.Salome Samwel wakati alipotembelea maonyesho ya biadhaa zao
yaliyokuwa katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini
Arusha.
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Bi. Daniela Schadt na Mwanamke mjasiriamali mwenye asili ya
Kimasai Bi. Salome Samwel wakiwa katika nyuso za furaha juzi jijini Arusha
wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa BEYOND 2015 unaoratibiwa na kutekelezwa
na DSW Tanzania.
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bi. Daniela Schadt akiangalia zawadi ya michoro ya kitamaduni aliyopewa na
Shirika la DSW Tanzania wakati wa hafla uzinduzi wa mradi wa BEYOND 2015 juzi jijini Arusha.
Aliyemshikia zawadihiyo ni Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga na Afisa
Miradi wa DSW Tanzania Bi. Diana Shuma
(mwenye shati jeupe).
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bi. Daniela Schadt (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la DSW Tanzania wakati wa hafla ya
uzinduzi wa mradi wa mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini Arusha.Waliokaa kutoka
kushoto ni Mke wa Balozi wa Ujerumani hapa nchini Bibi. Wenday Marshall –
Kochanke, Mkuu wa Wialaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe Munasa, Mkurugenzi wa DSW
Tanzania Bw. Peter Owaga na Mratibu wa Programu za Vijana kutoka Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii Dkt. Elizabeth Mapella. (Picha zote na Mpigapicha wetu, Arusha)
Na
Mwandishi Wetu, Arusha
MKE wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bi. Daniella Schadt ametoa wito kwa jamii
kuhakiksha wanatoa kipaumbele katika kushirikisha vijana kwenye nyanja
mbalimbali za maendeleo.
Wito huo umetolewa juzi
jijini Arusha wakati Mke huyo wa Rais wa Ujerumani alipokuwa akizindua mradi wa
utetezi na ushawishi wa jamii katika kutoa vipaumbele katika sekta za Elimu,
Afya na Ajira kwa vijana ujulikanao kama BEYOND 2015 ambapo mradi huo
unaratibiwa na Shirika lisilo la Kiserikali la DSW Tanzania.
Bi. Daniela alisema
kuwa jamii inapaswa kutoa mkazo katika sekta za Elimu, Afya na Ajira kwa vijana
kwa kuwa duniani kote vijana ndiyo nguvu kazi katika kuletea maendeleo ya taifa
lolote lile.
‘Tunapaswa kuweka mkazo
kwa vijana wadogo, maisha yao ya baadaye yanaanza kuanzia sasa, tuweke mkazo
katika Elimu na Afya kwa vijana wetu ili waeze kutambua fursa na kuzitumia.’’
Alisema Bi. Daniela.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa DSW Tanzania Bwana Peter Owaga amesema kuwa ni wao kama asasi ya kirai
wanashirikia na Serikali katika kuhakikisha utekelezaji wa sera zinazohusu
vijana nchini zinaleta tija.
Owaga ameongeza kuwa
Serikali kama msimamizi imepiga hatu kubwa kwa kuwa na Sera na miongozo mbalimbali
inayohusu vijana kama vile Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 inayotoa
fursa kwa kijana kujitambua.
Aidha Owaga aliongeza
kuwa mradi wa BEYOND 2015 ambao umezinduliwa na Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi.
Daniela Schadt umelenga kuongeza ushawishi na hamasa kwa washirika wa maendeleo
ili kutoka kipaumbele kwa kutenga bajeti kwa ajili ya Elimu , Afya ya Uzazi na
Ajira kwa vijana.
Akizungumzia mikakati
na namna mradi huo utakavyotekelezwa Afisa Muhamasishaji na Mawasiliano Bi.
Ester Mwanjesa amesema kuwa mradi huo utatekelezwa kwa mwaka mmoja katika mikoa
yote nchini ambapo mijadala mbalimbali itakuwa ikifanyika ili kuongeza hamasa
ya uashawishi utakaopelekea kutoa kipaumbele kwa vijana hususan katika nyanja
za Elimu, Afya ya uzazi na Ajira.
Mradi huu wa BEYOND
2015 ambao ni kifupi cha maneno Building
Expert Youth and Organisation for National Postion on the Post 2015 Development
umelenga kutatua changamoto za vijana asa baada ya kumalizika kwa muda wa
Malengo ya Melenia mapema mwaka huu.
No comments:
Post a Comment