TANGAZO


Friday, February 13, 2015

PSPF watoa mafunzo kwa Askari na watumishi Raia Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam

Ofisa Matekelezo Mwandamizi (SCO) wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Matilda A. Nyallu akitoa elimu ya Mpango wa Uchangiaji wa Hiyari kwa Askari na watumishi raia Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani, jijini Dar es Salaam.
 
Askari na watumishi raia wakifuatilia elimu hiyo iliyokuwa inatolewa na Maofisa wa PSPF, waliofika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani kutoa elimu ya Mpango wa Uchangiaji wa hiyari

Na Bakari Ngamba
MFUKO wa penseni wa PSPF ulipata fursa ya kukutana na kutoa elimu kuhusu huduma mbalimbali wanazozitoa na kuweza kuwapa maelezo ya baadhi  ya mafao yanayo tolewa kupitia  Mpango wa Uchangiaji wa Hiyari wa (PSS)  kwa Askari na watumishi raia makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam.

Bi. Matilda A. Nyallu ambaye ni Ofisa Matekelezo Mwandamizi (SCO) wa mfuko wa PSPF  aliweza kutoa rai kwa Askari na watumishi raia wote waweze kujiunga na mfuko wa jamii wa PSPF ili kuweza kupata mafanikiona kunufaika.
Pia alitoa mifano michache kwa ambao watajiunga  na mfuko huo ambapo kwa Askari na watumishi raia alitaja kuwa wanaweza kupata  mikopo ya kuanzia maisha ambayo itawawezesha kupata nyumba ambazo wamezijenga kwa ajili ya Mtanzania aweze kununua au kukopeshwa na baadaye kuweza kurejesha mkopo huo wa nyumba. 
Pia aliongeza kwa kusema nyumba zote zimewekewa bima endapo tatizo lolote likitokea basi nyumba hizo zitakuwa salama.
Hata hivyo, Ofisa wa Mfuko wa Pensheni Bw. Hadji Jamadary aliweza kuwaasa na kuwasisitiza mambo mbalimbali yanoyo tekelezwa na mfuko na kuwataka wawe miongoni mwa watu wenye muamko wa kujiunga ili wengine waweze kuiga mfano kutoka kwao.

Mfuko wa pensheni ni mfuko wa kijamii unao toa huduma na kukidhi mahitaji ya jamii paspo na gharama zinazo iumiza jamii , kujiunga na mfuko wa PSPF ndiko kutakako kuokoa katika kukuwekea dhamana ya maisha yako iwe ni katika elimu ,makazi,ugonjwa na hata ujasiliamali.

No comments:

Post a Comment