TANGAZO


Friday, February 13, 2015

Profesa Lipumba ayasitisha maandamano ya Vijana wa chama CUF (Juvicuf) jijini Dar es Salaam leo

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuahirishwa kwa maandamano ya vijana wa chama hicho, yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo jijini. kushoto ni Mwenyekiti wa Vijana wa CUF (Juvicuf), Hamidu Bobal. (Picha na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Na Celina Mathew
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesalimu amri kwa kukubali kutii amri ya Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kusitisha maandamano yao.

Akizungumza  Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba alisema hatua hiyo imekuja baada ya jeshi la polisi kuwataka wasitishe maandamano hayo ili kuepukana na dhana ya kupigwa kwa wafuasi wa chama hicho.

Alisema baada ya kupata taarifa kuwa polisi wamezuia maandamano hayo, alizungumza na vijana na kuwataka kusitisha suala hilo kwa kuwa hawakua na sababu ya kupinga zuio hilo la kufanya maandamano.

"Tumeona tusipinge zuio hilo, maana vijana wangeweza kupigwa risasi, kukamatwa au kupigwa mabomu hali ambayo ingewasababishia matatizo makubwa,"alisema.

Aliongeza kuwa leo asubuhi, alimpigia simu kamanda kova kuwa yeye na vijana wake wamesitisha maandamano ili polisi wasipige watu au kuwadhuru kwa namna yoyote.

Akizungumzia lengo la maandamano hayo alisema ni kushinikiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)kuongeza muda wa watu kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Lipumba alisema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Julai 9 mwaka jana zilisema kuwa vituo vya kupiga kura vitakuwea 4015 ambapo kila kituo kitaandikisha watu kwa siku 14 ambapo zilidai kuwa mchakato huo ungeanza Septemba mwaka jana ambapo haukuanza kutokana na vifaa havikufika.

"NEC walianza baadhi ya kata katika majimbo matatu ya Kawe, Kilombero na Katavi ambapo wangeandikisha kwa siku saba, jana tulipokutana walisema katika eneo la Kawe mchakato huo ulifanyika kata ya Mbweni na Bunju ambapo wapiga kura 15,123 waliandikishwa na kwamba lengo lilikuwa ni kuandikisha watu 14,312,"alisema.
Alisema kata hizo zilifanya majaribio na jumla ya watu 51,877 walijiandikisha na kwamba hawakuchukua watu waliohamia bali waliokuwepo kwenye sensa, ambapo sensa ilionesha jumla ya watu ni zaidi ya elfu 51.
"Kutokana na dhana hiyo zaidi ya asilimia ya lengo ni dhahiri kuwa wananchi wengi hawajajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura hivyo watapoteza haki zao za msingi,"alisema.

Aidha alisema takwimu zinaonesha wasiwasi una msingi muhimu na kwamba hadi sasa ni tiketi 250 ambapo kwa mwaka huu itakuwa ni watu zaidi ya bilioni 23 hivyo qwapiga kura ni wengi zaidi ya waliopo kwenye daftari.

"Tunachotaka NEC itoe muda wa kutosha ili wananchi waweze kujitkeza kujiandikisha, tume haifanyi kazi kwa wakati, hata ukiangalia kwenye tovuti hakuna taarifa kuhusu uandikishaji,"alisema.

Aliongeza kuwa kutokana na utendaji mbaya wa NEC unaweza kusababisha vijana wasijiandikishe na hoja ya msingi ni tume hiyo kutofanya kazi kwa wakati maalum.

"Wananchi wengi wanajishughulisha na kilimo hivyo muda wa siku saba wa kujiandikisha hautoshi, tume iongeze muda ili kila mwananchi aweze kujindikisha,"alisema.

Akizungumzia kura ya maoni Lipumba alisema mchakato huo hauwezi kukamilika kwa sasa kutokana na watu wengi hawajajiandikisha na kwamba watu wote Milioni 23 hawawezi kujindikisha kwa muda mmoja.

"Mchakato wa kura ya maoni hauwezi kufanyika kwa sasa, kwasababu watu wengi hawajajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, hivyo NEC ijipange upya itenge muda maalumu kwa ajili ya mchakato huo,"alisema.

No comments:

Post a Comment