Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana (kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa 'Mpe Riziki si Matusi" kumlinda mwanamke dhidi ya ukatili katika masoko wakati akiuzindua Dar es Salaam jana. Mradi huo unaendeshwa na Shirika la Equality for Growth (EfG). Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Ilala, Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Wilaya ya Ilala, Nora Mzeru.
Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita (kushoto), akimkaribisha Naibu Waziri Dk. Pindi Chana baada ya kuwasili kwenye uzinduzi wa mradi huo.
Baadhi ya maofisa wa EfG (wenye sare) na wadau wengine wakisakata rhumba kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita (katikati), akitoa hutuba fupi mbele ya mgeni rasmi, Naibu Waziri Chana Pinda (kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Wilaya ya Ilala, Nora Mzeru.
Baadhi ya wenyeviti wa masoko mbalimbali ya Manispaa wa Ilala, wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mmoja wa wadau waliofadhili mradi huo, akisalimia wageni
waalikwa.
Wanawake wafanyabiashara kwenye masoko mbalimbali wakimsikiliza mgeni rasmi Dk. Pinda Chana.
Mgeni rasmi Dk. Pindi Chana (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanawake wafanyabiashara masokoni na wadau wengine baada ya kuzindua mradi huo.
Hapa ni burudani kwa kwenda mbele.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Wilaya ya Ilala, Nora Mzeru (kushoto), akizungumza kwenye uzinduzi huo. (Kwa hisani ya Dotto Mwaibale wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment