*Ni kupitia promosheni ya JayMillions
*Bilioni 24.3 zawasubiri wateja
Mshindi wa kitita cha Shilingi Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hynes Kanumba ambaye ni mkazi wa Inyonga Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya NMB tawi la Mpanda baada ya kukabidhiwa fedha zake na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (kulia) Hafla hiyo ilifanyika katika tawi hilo mkoani humo. Ili kujua mteja kama umeshinda tuma neno Jay kwenda 15544.Meneja wa benki ya NMB mkoa wa Katavi Erick Luanda akimuonyesha taarifa za fedha ya benki (bank statement) Mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania , Hynes Kanumba mkazi wa Inyonga Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi(wapili toka kushoto) wanao shuhudia ni Meneja mauzo wa Vodacom kanda ya Kusini Petro Chinyama(kusho) na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu(kulia)Ili kujua mteja kama umeshinda tuma neno Jay kwenda 15544.
Mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hynes Kanumba ambaye ni mkazi wa Inyonga Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi akiwa anaondoka na mtoto wake mgongoni baada ya kukabidhiwa kitita chake rasmi na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(hayupo pichani) kwenye ofisi za benki ya NMB tawi la Mpanda mkoani humo mwishoni mwa wiki. Ili mteja kujua kama umeshinda tuma neno Jay kwenda 15544.
Hayawi hayawi yamekuwa Haynes Peter Kanumba(20) ambaye ni mshindi wa Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa kitita chake na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi iliyofanyika mkoani Katavi.Ili mteja kujua kama umeshinda unatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Mshindi wa Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hynes Kanumba mkazi wa Inyonga Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi akipongezwa kwa kupigiwa makofi na Meneja Uhusiano wa Vodacom Matina Nkurlu (kulia) Meneja Mauzo wa kampuni hiyo wa kanda za juu kusini na Meneja wa NMB mkoa wa Katavi Erick Luanda,mara baada ya kumkabidhi kitita chake wakati wa hafla fupi iliyofanyika mkoani Katavi mwishoni mwa wiki.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kulia) akimkabidhi kitita cha shilingi Milioni 10/- Hynes Kanumba ambaye ni mkulima mkazi wa Inyonga mkoa wa Katavi,alizojishindia kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika tawi la NMB Mpanda mkoani Katavi mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia katika picha kutoka kushoto ni Meneja wa NMB mkoani humo Erick Luanda,Meneja mauzo wa kampuni hiyo wa Kanda za juu kusini Petro Chinyama . Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Na Mwandishi wetu
MMOJA wa washindi wa milioni 10 kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania – Hynes Petro Kanumba mkazi wa Katavi mwishoni mwa wiki alikabidhiwa fedha zake katika hafla iliyofanyika mkoani humo.
Promosheni ya Jaymillions inayoendelea ikiwa katika wiki ya tatu na ambayo itadumu kwa muda wa siku 100 itaendelea kuleta faraja na mafanikio kwa wateja wa Vodacom kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha.
Hadi kufikia leo ni Sh. 126m/- pekee zilizokwisha kuchukuliwa na Uwezo Madengenya na washindi wengine wawili – Hyness Petro Kanumba kutoka Rukwa na James Mangu (Mwanza) – wa Sh. 10m/- na milioni 6m/- zimekwenda kwa – Chiliphod Wanjala (Mwanza), Janeth Nganyange (Njombe), Evarista A (Mwanza), Stanley Bagashe (Shinyanga), Ramadhani H. Maulid (Dodoma) na Lucas Masegese (Shinyanga) – wa Sh. 1m/-. Kiasi cha zaidi ya Sh. 5bn/- (ambazo ni sawasawa na magari madogo 428 ya muundo wa mgongo wa kobe) zingeweza kunyakuliwa na wateja iwapo wangetuma neno “JAY” kwenda 15544 kucheki kama wameshinda.
Akizungumza wakati akikabidhiwa fedha zake za Ushindi, mshindi wa Shilingi Milioni 100 wa Promosheni hiyo, Hynes Kanumba, amewaomba Watanzania kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Kampuni ya Vodacom nchini katika kujenga na kuimarisha maisha ya Watanzania.
"Promosheni ya Jaymillions naona inalenga kuwakomboa kimaisha watanzania hususani wenye kipato cha chini hasa wajasiriamali wadogo wadogo kama vile; wamachinga, mama ntilie, na wazee wastaafu ambapo kwa kiasi kikubwa tunajua watu wa aina hii wanahitaji msaada ili kujiendeleza kiuchumi. Kwa fedha ambazo baadhi ya washindi tayari wamezipata wengi zimewasaidia kujikwamua na kujiendeleza kimaisha," alisema Kanumba.
"Promosheni ya Jaymillions naona inalenga kuwakomboa kimaisha watanzania hususani wenye kipato cha chini hasa wajasiriamali wadogo wadogo kama vile; wamachinga, mama ntilie, na wazee wastaafu ambapo kwa kiasi kikubwa tunajua watu wa aina hii wanahitaji msaada ili kujiendeleza kiuchumi. Kwa fedha ambazo baadhi ya washindi tayari wamezipata wengi zimewasaidia kujikwamua na kujiendeleza kimaisha," alisema Kanumba.
Aliongeza kuwa yeye ni mfano dhahiri wa Watanzania kuwa promosheni hii haina ujanja bali ya kweli kwa kuwa pamoja na kuishi kijijini ameweza kushinda na leo ameingiziwa fedha zake kwenye akaunti. "Sasa nimepata mwanga katika maisha yangu baada ya kujishindia fedha hizi kwa sababu sijapewa masharti wala utaratibu wowote wa matumizi ya fedha hizi, maisha niliyokuwa nayo yalikuwa duni sana ambayo yamewezeshwa na promosheni hii’’.Alisema.
Kanumba alisema ndoto yake ya kuwa mkulima stadi anayejimudu imetimia kwa kuwa kwa muda mrefu amekuwa akifanya kazi ya kilimo akiwa anakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile kutokuwa na pembejeo za kisasa ili niweze kuendesha kilimo cha kisasa “Kuanzia sasa kwa fedha nilizopata nitamaliza shughuli zangu za kilimo na nitanunua mifugo na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili familia yangu.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, akiongea katika hafla hiyo alimpongeza mshindi huyo na kusema kwamba fedha hizo zimeenda kwa mshindi sahihi kwani mshindi huyo ana malengo mazuri ya matumizi ya fedha zake kwa kuendeleza kilimo cha kisasa kwani kilimo ndiyo uti wa mgongo kwa Taifa letu.
Pia aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni ya Jaymiilions ili wajishindie mamilioni ya fedha kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza bahati zao za kushinda.Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-
“Tunaendelea kuwasisitizia wateja wetu wacheki kila siku ili kujua kama namba zao zimeshinda. Kama Kanumba asingetuma ujumbe siku ile angeendelea tu na maisha yake kama yalivyokuwa bila kujua kama namba yake ilichaguliwa kushinda. Hadi hivi sasa tuna washindi 10 wa zawadi za pesa taslimu Sh. 127m/- lakini kila siku wateja 111 wanachaguliwa kushinda. Bado kuna Sh. 24.3bn/- za kushindaniwa kwa siku 79 zilizosalia kwenye promosheni hii hivyo endeleeni kutuma “JAY” kwenda 15544 kila siku,” alisema Nkurlu.
Pamoja na mambo mengine benki ya NMB imejitolea kutoa mafunzo ya ujasiriamali na matumizi sahihi ya fedha kwa Mshindi huyo ili kumuwezesha kuwa na matumizi yenye tija.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika tawi la benki ya NMB Katavi, Meneja wa tawi hilo Erick Luanda alisema kuwa benki yake imekuwa na ushirikiano mzuri wa kibiashara na hiyo hasa kupitia huduma yake ya M - pesa.
Luanda aliongeza kuwa mshindi wa Jaymilion pia ana akaunti na NMB hivyo kufanya benki kuamua kumpa ushirikiano mteja wao kwa kumkabidhi fedha zake kwenye ofisi za NMB.
"kwanza ukiangalia huyu ni mteja wetu, pili sisi tumekuwa na uhusiano mzuri na kampuni ya Vodacom, Hivyo tumeona ni vyema kutumia fursa hii kutoa elimu kwa mshindi wa promosheni hii ili kumuwezesha awe na matumizi sahihi ya fedha yatakayo leta tija katika maisha yake,” alisema Luanda na kuongeza kuwa wataalamu wa benki watampatia elimu ya ujasiriamali ili aweze kujiendeleza kutokana na fedha alizopata.
No comments:
Post a Comment