TANGAZO


Sunday, February 8, 2015

Redd's Miss Tanzania 2013, Happyness Watimanywa afungua Klabu ya kujisomea watoto wa Nkema

Redds Miss Tanzania 2013, Happness Watimanywa (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Club ya kujisomea watoto ya ijulikanayo kwa jina la Nkema Reading Club iliyopo Kinondoni Mtaa wa Kasana jirani na Kituo kinachojengwa kwa ajli ya Mabasi ya Mwendokasi nyuma ya Sheli ya Mwanamboka katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo, Getrude Kilyabusebu.
Redds Miss Tanzania 2013, Happyness Watimanywa (kushoto), akiwafundisha kusoma watoto wakati wa hafla ya kufungua Club ya  kujisomea watoto ya Nkema Reading Club iliyopo Kinondoni Dar es Salaam juzi ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Redds Miss Tanzania 2013, Happyness Watimanywa akiwa katika picha ya pamoja na watoto na wazazi wao wakati wa hafla hiyo.
 Mtoto Careen Elly akimlisha keki maalumu Redds Miss Tanzania, Happnes Watimanywa  iliyoandaliwa kwa ufunguzi wa Club hiyo.
Mtoto Kelvin Elly akichora picha mbalimbali kwenye chumba maalumu cha kujisomea watoto ndani ya Club hiyo.
Watoto wakijisomea vitabu mbalimbali ndani ya Club hiyo. Kutoka kushoto ni Hope Njau, Careen Elly na Angel Mtango.
Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo Getrude Kilyabusebu (katikati), akiwafundisha kusoma watoto hao.
Mmoja wa maofisa wa Club hiyo, Hilda Ngaja (kulia), akiwaelekeza jambo watoto hao.
Keki maalumu ya hafla hiyo ilivyokuwa ikionekana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo Getrude Kilyabusebu (katikati), akizungumza na wazazi watoto hao (hawapo pichani), wakati wa uzinduzi huo. Kushoto ni Mmoja wa maofisa wa Club hiyo, Rose Kelly na Redds Miss Tanzania 2013, Happyness Watimanywa.
Careen Elly (kulia), akimwelekeza mwenzake namna ya kuandika.
Redds Miss Tanzania 2013, Happyness Watimanywa akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa Club hiyo pamoja na wazazi wao.


Na Dotto Mwaibale
WAZAZI wametakiwa kutowaacha watoto wao kucheza baada ya muda wa masomo badala yake wawapeleke kwenye vituo vya kujisomea ili kupata maarifa zaidi.

Mwito huo umetolewa na Redds Miss Tanzania 2014, Happyness Watimanywa wakati wa hafla ya kufungua Club ya watoto ya kujisomea ya Nkema Reading Club iliyopo Kinondoni Dar es Salaam juzi ambapo alikuwa mgeni rasmi.

"Tunawaomba wazazi kote nchini wajenge tabia ya kuwapeleka watoto kwenye club za namna hiyo badala ya kuwaacha wakicheza" alisema Watimanywa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo Getrude Kilyabusebu alisema ameamua kuanzisha clabu hiyo ili kutoa fursa kwa watoto kujifunza mambo mabalimbali ambayo hawayapati katika shule zao.
"Tunahitaji watoto wajifunze mambo ya utamaduni wetu badala ya kuiga utamaduni wa nchi za nje ndio maana tumeanzisha club hii ambayo itakuwa inawakutanisha watoto siku ya Jumamosi ambapo watakuwa na uwezo wa kusoma bila kushurutishwa" alisema Kilyabusebu. 

Alisema watoto kushiriki katika club hiyo itawaongeza ujasiri na kujiamini katika masomo yao na hasa namna ya kujieleza mbele ya watu kwani hapa nchini kumekuwa na changamoto kubwa ya watoto na hata watu wazima kujieleza kwa ufasaha kwa lugha ya kiingereza na kiswahili mbele za watu tofauti na nchi zingine.

Mmoja wa wazaizi wa watoto hao Hellen Mwenda alisema club kama hiyo inawasaidia sana watoto kuwajengea uwezo wa kujiamini katika masomo yao kutokana na kuchanika na watoto wenzao.
Mwenda alisema pamoja na watoto kujifunza mambo mengine wakiwa shuleni kwao lakini kwa kuwapeleka katika club hizo wanapata vitabu ambavyo wanavikosa katika mashule yao.

Club hiyo ipo Kinondoni jirani na Vijana Social Hall ndani ya Ghorofa kilipo chuo cha Mweni Training College kwa maelekezo zaidi piga simu namba-0754-032589.

No comments:

Post a Comment