Vijana wa mafinga wakishangila
uwepo wa Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi, Miraji
Mtaturu.
Na Fredy Mgunda, Mufindi
HALMASHAURI ya mufindi
yapewa wiki 3 kujenga kizimba cha takataka soko kuu mafinga pia
kusambaza maji katika vyoo vya halmashauri vilivyopo sokoni hapo.
Wiki tatu hizo zimetolewa
na Katibu wa chama cha mapinduzi wilayani mufindi Miraji Mtatulu
baada ya kufanya ziara ya kushtukiaza katika soko hilo na kubaini
kuwapo kwa kizimba kinacho tumiwa kuhifadhi taka hakijajengwa kwa
utalamu ikiwa kinauchafu na maji ya muvua nayo yanapita hapo hali
inaypelekea kuhatalisha afya za wafanyabiashara katika eneo hilo
hususani mlipuko wa magonjwa.
Pia mtatulu ametoa wiki
tatu kwa halmashauri kukarabati miundo mbinu ya choo ambapo choo hiyo
imekuwa ikitumiwa pasipo maji huku usafi wake nao ukiwa hafifu na
kwaupande wa choo ya mtu binafsi ametakiwa kuweka maji vyooni na
kuboresha usafi ndani ya wiki hizohizo tatu.
Nao wafanyabiashara
wamemtaka kuchukua hatua stahiki kutokana na baadhi ya wataalamu wa
serikali kuchukulia maneno ya wanasiasa ni siasa pia kutakiwa
kuaahidi kama mambo hayo yasipofanyika ni hatua gani atachukua au
nini afanyiwe,
"Utatuaminisha vipi
kuwa wewe utalifanyia kazi suala hili ikiwa hawa wataalamu wengi wao
huamini maneno yanayozungumzwa na wanansiasa ni siasa" Akijibia
amesema Ilikuonyesha amejitoa kufanya kazi ya jamii yeye hana tofauti
na shehe,Mchungaji, au Padrii hivyo atahukumiwa siku ya mwisho hivyo
hawezi acha ahukumiwa kwasababu ya uzembe wa baadhi ya watendaji
waliopewa jukumu la kufanya kazi hiyo.
Kwa upande wa katibu wa
soko hilo FREDRICK MNG'ONG'O Ameibua changamoto ambayo kwasasa
iliyokuwa mupango wa wafanyabiashara hao kujakugomea kitendo cha
Serikali kupandisha kodi kwa asilimia mia huku TRA wakijipangia tuu
kiasi cha kulipia kuwa ni mara 2 ya malipo ya mwaka jana jambo ambalo
limewafanya wafanyabiasha wote kuitaka halmashauri kuandaa mkutano
utakaotolea ufafanuzi juu ya swala hilo ikiwa na kuanika hadharani
viwango vya ushuru kwa kila biashara ili kuondokana na rushwa za
lazima huku wakimtaka na katibu huyokuhudhuria kutoa ushauriwake.
Mara baada ya kikao katibu
amewataka wananchi kutokukichukia chama kilichopo madarakani kwani
wanaokifanya chama hichohicho kutopendwa ni wafanyakazi wa sekta
mbalimbali kutofanya kazi zao kwa maadili pia chama hicho hakiwatumi
watumishi hao kuwaibia wananchi kwa maana ya kuwafisadi
wananchi.
"Wananchi kwa pamoja tunatakiwa kuwawajibisha watendaji kwani wao ndio hawafanyikazi na chama kama chama kinafanya ipasavyo na sasa naanza na hawa ambao wao hawafanyi kazi za wananchi", alisema.
"Wananchi kwa pamoja tunatakiwa kuwawajibisha watendaji kwani wao ndio hawafanyikazi na chama kama chama kinafanya ipasavyo na sasa naanza na hawa ambao wao hawafanyi kazi za wananchi", alisema.
Katika kusisitiza na
kujazia kuwa lazima baada ya wiki tatu anakagua tena kama yametendewa
kazi amesema halmashauri inaweza kutumia fedha zitakazo ludishwa na
waliozichukua kauli hiyo ilishangiliwa na wafanyabiashara waliokuwapo
katika mkutano huo,kauli hiyo imekuja wakati baadhi ya wafanyakazi wa
halmashauri hiyo wakiwa wamefikishwa mahakama ya wilaya ya mufindi
kwa makosa ya uhujumuuchumi katika halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment