Kinara mkuu wa kundi la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram, Abubakar Shekau, ameapa kwenye mkanda wa video mapema Jumatatu kuwa, kundi hilo litashinda majeshi ya muungano mwa kanda hiyo yanayopania kukabiliana na kundi hilo kazkazini mashariki mwa Nigeria, Niger na Cameroon.
Abubakar Shekau anasikika akisema kuwa muungano huo hautaafikia lolote, ''toeni silaha zenu zote na muanze kutukabili,
Tunawakaribisha''
Alisema hayo katika mkanda huo wa video wa dakika ishirini na nane uliowekwa kwenye mtandao wa YouTube na kundi hilo la wapiganaji wa kiislamu.
Awali Bunge nchini Niger lilitangaza kupiga kura Hivi leo kuamua iwapo wanajeshi watatumwa kupigana na wanamgambo hao wa Boko Haram kama sehemu ya jitihada za kulishinda kundi hilo.
Kura hiyo inafanyika siku tatu baada ya Boko Haram kuendesha moja ya mashambulizi mabaya zaidi nchini Niger.
Mataifa jirani ya Nigeria wamejiunga kwenye harakati hizo wakati kundi hilo linapopanua operesheni zake kwenda Chad, Cameroon na Niger.
No comments:
Post a Comment