TANGAZO


Monday, February 9, 2015

Merkel kukutana na Obama kuhusu Ukraine

Mkutano wa kutafuta amani nchini Ukraine
Chancellor wa Ujerumani Angela Merkel, anatazamiwa kukutana na Rais wa Marekani Barrack Obama huko White House muda mfupi ujao, ili kufanya mazungumzo ambayo mzozo Nchini Ukraine unatazamiwa kuutawala mkutano huo.
Bwana Obama anaunga mkono juhudi za hivi punde za Ufaransa na Ujerumani kujaribu kutafuta suluhu ya kumaliza mapigano, kati ya serikali ya Ukraine makundi ya wapiganaji yanayoungwa mkono na Urusi.
Aidha bado kuna uwezekano wa Marekani kuamua kuipa silaha Ukraine, iwapo suluhu kamili ya kukomesha mapigano hayataafikiwa-- jambo ambalo Bi Merkel amesema huenda ikaharibu zaidi hali ya mambo.
Awali mawaziri wa Nchi za kigeni kutoka Jumuia ya bara Ulaya waliafikiana kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya Urusi na makundi yanayotaka kujitenga Nchini Ukraine -- lakini vikwazo hivyo havitaanza kutekelezwa mara moja hadi siku ya Jumatano pale mkutano mwingine wa amani utakapofanyika.
Kiongozi wa Ujerumani kukutana na rais Obama kujadiliana kuhusu amani Ukraine
Ukraine inasema kuwa zaidi ya wanajeshi elfu moja mia tano wakiwa na silaha nzito nzito wameingia mashariki mwa Ukraine mwishoni mwa juma.
Wakuu Nchini Ukraine wanasema kuwa wanajeshi zaidi wa Urusi wameingia mashariki mwa Ukraine wakiwa na vifaa vizito vya kijeshi.
Msemaji wa jeshi Mjini Kiev wanajeshi elfu moja na mia tano wa Urusi na vifaa 300 vya kijeshi, vinavyojumuisha mizinga ya masafa marefu, yalivukishwa mpaka mnamo siku ya Jumamosi na hapo jana Jumapili.

No comments:

Post a Comment