TANGAZO


Monday, February 9, 2015

Vifo uwanjani: Ligi kuu yasimama Misri

Mashabiki wanadai kuwa mamlaka zilisababisha vurumai zilizotokea baada ya kufungua lango moja pekee
Misri imesimamisha kwa muda usiojulikana ligi kuu ya nchi hiyo baada ya watu zaidi ya Watu 20 kufariki dunia.
Kati ya waliofariki ni wengi wao ni Mashabiki wa timu ya Zamalek ambao walifariki kutokana na msongamano wakati Polisi walipowafyatulia mabomu ya machozi baadhi ya mashabiki waliokuwa wakijaribu kuingia kwa nguvu ndani ya uwanja wakati timu hiyo ilipokuwa ikipambana na timu ya ENPPI.
Mtandao mmoja nchini humo uitwao AL-Misriyun umeripoti.Tukio hilo limetokea baada ya Polisi kutumia gesi ya kutoa machozi kuwasambaratisha mashabiki walikokuwa wakitumia nguvu kujaribu kuingia uwanjani.
Taarifa ya Wizara ya mambo ya ndani ya Misri inasema kuwa Mashabiki wa Zamalek walikuwa wanataka kuingia uwanjani kwa nguvu hivyo walikuwa wakiwazuia ili kunusuru mali ya uma isiharibike.
Polisi wamesema mashabiki hao walikuwa wanataka kuingia uwanjani bila tiketi, wamenukuliwa wakisema Watu hao walipoteza maisha baadhi kutokana na msongamano mkubwa wengine walipokuwa wakipambana na Polisi.
Ndani ya uwanja kulionekana rundo la viatu karibu na miili ya Watu waliopoteza maisha na wengine waliolala wakiwa majeruhi.
Mashabiki wa Zamalek wanadai kuwa vurumai zilianza mamlaka ya uwanja ilipofungua Geti la waya kuwaruhusu kuingia ndani.
Mashuhuda wanasema uzio ulianguka wakati Watu walipokuwa wakipigania kuingia ndani hali iliyosababisha msongamano mkubwa, mara askari wa usalama walianza kurusha mabomu ya kutoa machozi.
Watu walianza kukanyagana hali iliyosababisha Watu kupoteza maisha.
Tukio hili limetokea ikiwa ni miaka mitatu tangu Wapenzi wa soka zaidi ya 70 walipopoteza maisha wakati vurugu zilipotokea katika uwanja wa ndege wa Port Said.
Baada ya tukio hilo idadi maalum iliwekwa kwa watakaohudhuria Mechi kwa hofu ya hali ya usalama ,inaelezwa kuwa mipaka hiyo iliyoondolewa hivi karibuni huwenda ikawekwa tena baada ya tukio la mwishoni mwa juma lililopita.

No comments:

Post a Comment