TANGAZO


Friday, January 16, 2015

Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja Kichama

Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana, akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Rahaleo Mhe Abdalla Juma Mabodi, alipofika katika jimbo hilo kuzindua Mradi wa Maji Safi na Salama na kujionea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi yaCCM kwa Wananchi wa Jimbo hilo. (Picha zote kwa hisani ya ZanziNews)
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana, akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo, Mhe Nassor Salim Jazira, alipowasili katika Tawi la CCM Makadara chini,kuangalia utekelezaji wa Ahadi za Mbunge na Mwakilishi kwa Wanachi wa jimbo hilo na kuzindua mradi wa utandazaji wa mipira ya kusambazia maji kwa wananchi wa Shehia ya Makadara chini.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, akisalimiana na Wananchi wa Jimbo la Rahaleo alipowasili katika Tawi la CCM Makadara Chini, akiwa katika ziara yake kutembelea miradi na kuimarisha Chama na kujionea utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa wananchi wake.
 Mbunge wa Jimbo la Makadara Mhe Abdallah Juma Mabodi, akizungumza wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, alipofika katika Tawi la CCM Makadara, akizungumzia mafaniko ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika jimbo na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.  
Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe. Nassor Salim Jazira, akizungumza na Wananchi wa Jimbo lake wakati alipopewa nafasi ya kuelezea mafanikio ya Jimbo lake katika kufanikisha malengo ya miradi ya maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.  
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Abdulrahman Kinana akiwapongeza Mbunge na Mwakilishi wa Chama cha Mapinduzi kwa mafanikio ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa wananchi wa Jimbo lao wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo na kuimarisha Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abrahaman Kinana akishiriki katika ujenzi wa taifa katika jimbo la Rahaleo katika uchimbaji wa mtaro wa kutandaza mipira ya maji safi na salama kwa Wananchi wa Jimbo la Rahaleo shehia ya Makadara chini, mradi huo unatekelea Ilani ya Uchaguzi ya CCM na unasimamiwa na Mbenge na Mwakilishi wa jimbo hilo.wakiwa katika tawi la CCM Makadara.
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni wakisherehekea ujio wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi katika jimbo lao kujionea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, akiwa katikaxziara yake katika Mkoa wa Mjini Unguja, wakati alipofika kuangalia ujenzi huo wa kituo cha Afya cha jimbo hilo Shehia ya Miembeni.  
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abrahaman Kinana na ujumbe wake wakimsikiliza msoma taarifa wa Jimbo la Kikwajuni Ndg. Jacob Joseph. alipotembelea kuona utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kuwaletea huduma ya Afya Wananchi karibu na makaazi yao. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abrahaman Kinana akijenga taizi wakati alipotembelea kuona utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa ujenzi wa hospitali ya Jimbo la Kikwajuni unaojengwa na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe Mahmoud Muhammed Mussa, kwa ajili ya kutowa huduma za afya kwa Wananchi wa jimbo hilo na jirani zao Ndg Kinana ameahidi kutoa mifuko 50 ya saruji na taizi boski 50 kwa ajili ya umaliziaji wake akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abrahaman Kinana akionesha mandhari ya mitaa ya vikokotoni na akiwa juu ya jengo la mradi wa maduka baada ya kulizindyua jengo hilo.akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa Tawi la CCM Vikokotoni Ndg. Ali Hassan, na anayefuatia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Vuai Ali Vuai. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Vuai Ali Vuai, akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abrahaman Kinana akitembelea jengo la maduka la mradi wa Tawi la CCM Vikokotoni la jimbo  Mkongwe baada ya kulizindua rasmin wakati wa ziara yake, ya siku kumi Unguja na siku tano kisiwani Pemba.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi akiondoka katika Tawi la Chama cha Mapinduzi Vikokotoni baada ya kufungua jengo la Mradi wa tawi hilo la maduka katika mtaa wa Vikokotoni Unguja akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Mjini. kushoto Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM Ndg. Nape Mnauye na kulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg, Vuai Ali Vuai.

No comments:

Post a Comment