Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, akimkabidhi zawadi mmoja wa viongozi wa Benki ya Badea, wakati alipoufunga mkutano wa Kimataifa wa uwekezaji wa nchi za Huba na Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, akifurahi jambo na mmoja wa viongozi wa Benki ya Badea, wakati alipoufunga mkutano wa Kimataifa wa uwekezaji wa nchi za Huba na Tanzania, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mkutano huo, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima alipokuwa akiufunga rasmi leo.
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
SERIKALI ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kuendeleza ushirikiano na mahusiano mzuri uliopo kati yake na nchi zinazounda umoja wa nchi za Ghuba (GCC).
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alipokuwa akifunga mkutano wa siku mbili wa wafanyabishara kutoka Tanzania na nchi za GCC ambao ulianza Januari 15 hadi 16 mwaka huu.
Malima alisema kuwa Watanzania umefika wakati wa kuboresha biashara zetu ili kuweza kuuza bidhaa bora ndani na nje ya nchi na kukabiliana na changamoto za soko la kimataifa.
“Viwango vya mazao yetu vinapaswa viewe bora, ambapo ubora huo utaruhusu bidhaa zetu ziuzike nchi nyingine” alisema Malima.
Akitolea mfano, Malima alisema Tanzania imejaliwa kuwa na mifugo mingi inayoweza kuzalisha nyama ambayo soko lake tunalo tayari ambalo ni nchi za GCC na kusisitiza kuwa nyama hiyo inapaswa kuandaliwa katika machinjio salama na ya kimataifa ili kufungua fursa ya kuuza nyama hiyo maana milango sasa ipo wazi kwa serikali ikishirikiana na wafanyabiashara nchini.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara kutoka nchi za Ghuba (FGCCC) Abdulrahman Bin Saleh Al- Otainshan alisema kuwa jumuiya ya wafanyabiashara wan chi za Ghuba wameona na wanatarajia kufanya biashara Tanzania katika sekta ya kilimo na mifugo ambapo wanategemea kupata mzao mbalimbali yanayohitajika nchi za Uarabuni.
Mazao hayo yanayohitajika ni pamoja na mchele, matunda, mboga mboga, asali na nyama.
Zaidi ya hayo, Rais hyo wa FGCCC alisema kuwa nchi zianazounda umoja huo zinatarajia kuwekeza Tanzania katika sekta za kilimo, mifugo, elimu, maji, afya, ufundi na utalii.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa benki ya BADEA alisema kuwa Abdel Aziz Khelef alisema kuwa benki yake itaendelea kuwa kiunganishi muhimu kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na nchi za GCC ambapo wamekuwa na uhusiano mzuri kwa zaidi ya miaka 40.
Nchi zinazounda umoja wa GCC ni Kuwait, Oman, Bahrain, Qatar, UAE na Saud Arabia zinauhusiano wa karibu na Tanzania kihistoria, lugha pamoja mila na desturi.
No comments:
Post a Comment