TANGAZO


Friday, January 16, 2015

Rais Dk.Jakaya Kikwete akutana na wajumbe wa Jopo la Kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)

Rais Dkt. Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na wajumbe wa Jopo la Kutathmini Programu  ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN Independent Review Panel) linaloongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana Mheshimiwa Dkt. Festus Mogae ( aliyekaa wa kwanza kulia kwa Rais Kikwete) huko Ikulu tarehe 16.01.2015.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi tuzo maalum ya Vision 2025 Big Results Now kwa Rais Mstaafu wa Botswana Mheshimiwa Dkt. Festus Mogae aliyeongoza jopo maalum la kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa huko Ikulu tarehe 16.01.2015. 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi tuzo maalum ya Vision 2025 Big Result Now kwa Dkt. Sipho Moyo, Mkurugenzi Mtendaji wa ONE wa Kanda ya Afrika aliyekuwa miongoni mwa wajumbe wa jopo la kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa. Rais Kikwete aliwakabidhi tuzo hizo huko Ikulu tarehe 16.01.2015.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi Tuzo Maalum ya Vision 2025 Big Results Now kwa Bwana James Adams, Makamu wa Rais Mstaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa miongoni mwa wajumbe wa Jopo la Kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) huko Ikulu tarehe 16.01.2015.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal wakipiga picha ya pamoja na wajumbe wa Jopo la Kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN Independent Review Panel). Kulia kwa Mheshimiwa Rais Kikwete ni Rais Mstaafu wa Botswana Dkt. Festus Mogae akifuatiwa na Bwana James Adams (Makamu wa Rais Mstaafu wa Benki ya Dunia), aliyesimama wa kwanza kushoto ni Bibi Linah Mohohlo (Gavana wa Benki Kuu ya Botswana) na wa kwanza kulia ni Dkt. Sipho Moyo (Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Afrika, ONE. Waliosimama mstari wa nyuma (kulia kwenda kushoto) Dkt. Nkosana Moyo (Mwanzilishi wa Mandela Institute for Development Studies) akifuatiwa na Lord Peter Mandelson (Mwenyekiti, Global Counsel ‘Uingereza’), anayefuata ni Bwana Knut Kjaer, (Mwenyekiti, Trident Asset Management, ‘Norway’). (Picha zote na John Lukuwi) 

No comments:

Post a Comment