TANGAZO


Saturday, January 17, 2015

Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana Zanzibar

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia maziwa yanayotengenezwa katika Kiwanda kipya cha Azam Dairy Products Limited, alipokwenda kutembelea kiwanda hicho eneo la Fumba, Unguja Zanzibar jana wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya uchaguzi ya CCM. 
Kinana akikata utepe kuzindua rasmi gari la kubebea wagonjwa lililotolewa na Mbunge wa Jimbo la Fuoni, kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa katika jimbo hilo. Hafla hiyo ilifanyika Zanzibar leo. 
Kinana akishiriki kufyeka majanI mbele ya Chuo cha Sayansi ya Bahari (IMS), alipotembelea chuo hicho kilicho chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam eneo la Buyu, Unguja Zanzibar leo. 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanda samaki aina ya kaa katika shamba la ushirika Jimbo la Fuoni, Unguja Zanzibar leo. 
Kinana akikata utepe kuzindua rasmi gari la kubebea wagonjwa lililotolewa na Mbunge wa Jimbo la Fuoni, kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa katika jimbo hilo. Hafla hiyo ilifanyika Zanzibar leo. (Picha zote na Richard Mwaikenda)

No comments:

Post a Comment