*Chakaribisha wawekezaji binafsi ujenzi wa Hosteli za wanafunzi wa kike
*Naibu Waziri Mhagama atunuku wahitimu 374
Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), wakiwa kwenye mahafali yao, ambayo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama aliwatunuku wahitimu 374 Shahada mbalimbali.Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), wakiwa kwenye mahafali yao hayo.
Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), wakiwa kwenye mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), wakiwa kwenye mahafali yao.
Na Richard Mwangulube, Arusha
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenista Mhagama(mb) leo ametunuku Astashahada, Stashahada na Shahada kwa wahitimu wapatao 374 katika chuo cha ufundi arusha—ATC.
Kati ya wahitimu hao 334 ni wanafunzi waliohitimu astashahada na stashahada katika fani ya sayansi, teknolojia na uhandisi sanifu.
Aidha, wanafunzi 24 wamehitimu shahada katika uhandisi ujenzi umwagiliaji, 13 wamehitimu katika programu ya teknolojia Sayansi za maabara.
Aidha wanafunzi 17 wamehitimu katika masuala ya ufundi sanifu uhandisi umeme na elektroniki.
Akizungumzia program ya ya teknolojia ya sayansi za maabara, Naibu Waziri Mhangama amesema program hii ni muhimu wakati huu serikali ya awamu ya nne imeamua kujenga maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi katika kila shule ya Sekondari.
Naibu Waziri Mhagama amefafanua kwamba hivi sasa kuna upungufu mkubwa wa wataalam wa eno hili katika shule zote za Sekondari.
Amesisitiza kwamba kuanzishwa kwa program hii na chuo cha ufundi Arusha itakwenda sanjali na makakati wa serikali swa kujenga maabara katika shule zote za Sekondari hapa nchini.
Amesema kuna mahitaji makubwa ya watalaam wa eneo hili katika shule zote za Sekondari nchini.
Amesisitiza kwamba wataalam hawa wataweza kufundisha kwa vitendo masomo yote ya sayansi pamoja na kuvifanyia matengenezo vifanyy hivyo pindi vikiharibika.
Pamoja na kutunuku rasmi astashahada, stashahada na shahada katika chuo hicho Naibu waziri huyo wa elimu na mafunzo ya ufundi amesema pia kuwa wahandisi wa sayansi na teknolojia ni muhimu katika karne hii ya mageuzi ya sayansi na teknolojia duniani.
Hata hivyo Naibu Waziri Mhagama ametaka na kusisitiza kuwepo na uwiano kati ya mafundi sanifu na wahandisi katika kuleta maendeleo ya nchi na mageuziya uchumi nchini.
Amesema makundi haya mawili ni makundi ambayo yote hutegemeana katika utekelezaji wa kazi zao za kila siku za miradi ambapo bila mafundi sanifu wahandisi kamwe hawawezi kutekeleza miradi.
Amesema Tanzania bado inakabiliw ana upungufu mkubwa wa mafundi sanifu na wahandisi hasa katika kutekeleza uhandisi ujenzi na umwagiliaji katika sekta ya kilimo
Naibu Waziri huyo amesema uhandisi ujenzi na umwagiliaji ni muhimu katika kupanua eneo la umwagiliaji hapa Tanzania.
Hivyo chuo cha ATC ni nguzo muhimu sana katika uendeshaji wa program hii hapa Tanzania ambapo program mbalimbali zinazotolewa na chuo hiki zinalenga kuwawezesha wahitimu kujiajiri.
Amepongeza jitihada zinazofanya na chuo cha ATC katika kuendesha program mbalimbali ambapo amesema bado Tanzania kuna mahitaji makubwa ya mafundi sanifu kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya maendeleo ya elimu na mafunzo na ufundi.
Akizungumza wakati wa mahafali hayo Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho Abraham Nyanda amesema program ya ufundi sanifu hasa ya uhandisi,sayansi na teknolojia na kilimo zinamahitaji makubwa nchini.
Mwenyekiti huyo ameiomba serikali kuipa kipau mbele kwa kukiongezea raslimali fedha chuo hicho.
Nyanda ametoa wito kwa wawekezaji binafsi kuwekeza katika chuo hicho katika ujenzi wa mabweni na hosteli hususani hosteli na mabweni ya wanafunzi wa kike.
Hatua hii itakiwezesha chuo kuchukua wanafunzi wengi wa kike wapatao 500 wanaotimkiza vigezo wakati wa udahili ambapo hivi sasa wanafunzi wengi w akike huachwa kutokana na umkosefu wa mabweni kwa ajili ya malazi.
Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Dkt Richard Masika amesema kati ya wanafunzi 374 waliohitimu mafunzo leo kati yao wahitimu 81 saw ana asilimia 21.7 ni wanafunzi wa kike.
Dkt Masika pia amesema kuwa chuo kimepanga kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka idadi ya sasa ya wanafunzi 1,605 hadi 3,000 mwaka 2018/19.
Mkuu huyo wa chuo pia ameeleza katika hotuba yake hiyo kwamaba Chuo kimepanga kuongeza program mpya kulingana na mahitaji ya taifa na soko la ajira.
Amezitaja program zinazotarajiwa kuanzishwa kuwa ni program ya Gesi na mafuta ambayo italenga kuwapa ujuzi wahitimu katika suala la usambazaji na matumizi sahihi ya bidhaa hiyo katika jamii.
Program nyingine ni ya teknolojia ya sayansi za maabara za mahospitalini ambapo chuo kwa mara ya kwanza chuo kimdto wahitimu wa ufundi sanifu katika uhandisi umeme na vifaa vya tiba.
No comments:
Post a Comment