TANGAZO


Saturday, January 17, 2015

Mali: Mwanajeshi wa kulinda amani auawa

Wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa wabeba jeneza la mwenzao aliyeuawa
Afisa mmoja wa kikosi cha kulinda amani katika Umoja wa Mataifa ameuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo kazkazini mwa Mali.
Millio ya risasi ilisikika karibu na kambi ya umoja wa mataifa ya wanajeshi wa Ufaransa katika mji wa Kidal.
Wakaazi wamesema kuwa walipuaji wawili wa kujitolea muhanga walishambulia kambi hiyo ya umoja wa mataifa na mabomu yaliotegwa ndani ya magari na kumuua afisa mmoja wa kikosi cha kulinda amani kutoka Chad na kumjeruhi afisa mwengine mmoja.
Oparesheni iliyoongozwa na Ufaransa mwaka 2013 ilifanikiwa kuwandoa wapiganaji ambao walikuwa wameliteka eneo la kazkazini,lakii wanamgambo hao wameimarisha mashambulizi yao katika miezi ya hivi karibuni.
Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Mali na wapiganaji wanaotaka kujitenga kuhusu hatma ya jimbo hilo yanaatarajiwa kuanza tena mjini Algiers.

No comments:

Post a Comment