TANGAZO


Thursday, December 18, 2014

Uzinduzi wa Umeme Kijiji cha Dongongwe Kati Unguja leo

Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban, akizungumza alipkuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kuzungumza na wananchi baada ya kuzindua rasmi nishati ya Umeme katika Kijiji cha Dongongwe, Wilaya ya Kati Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini Unguja leo. (Picha zote na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa wananchi wa Kijiji cha Dongongwe, Wilaya ya Kati Jimbo la Uzini, Mkoa wa Kusini  Unguja katika sherehe za Uzinduzi wa Umeme Kijijini hapo leo. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban, Mbunge wa Jimbo la Uzini Mohamed Seif Khatib (wa kwanza kulia), akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kusini Unguja, Ramadhan Abdalla Ali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa wananchi wa Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini  Unguja katika sherehe za Uzinduzi wa Umeme Kijijini hapo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZEC), Hassan Ali Mbarouk wakati alipofika Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Unguja leo kuzindua Nishati ya Umeme.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamed Raza wakati alipofika Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Unguja leo kuzindua Nishati ya Umeme.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZEC), Hassan Ali Mbarouk (katikati), wakati alipofika Kijiji cha Dongongwe, Wilaya ya Kati Unguja leo kuzindua Nishati ya Umeme. Kulia ni Waziri  wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban, Mbunge wa Jimbo la Uzini, Mohamed Seif Khatib na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk. Idriss Muslim Hija.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuzindua Nishati ya Umeme Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Unguja leo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dk. Idriss Muslim Hija (wa tatu kulia), Waziri  wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban, Mbunge wa Jimbo la Uzini Mohamed Seif Khatib na Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZEC) Hassan Ali Mbarouk.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiingiza namba katika kufungua pazia kuzindua, Nishati ya Umeme Kijiji cha Dongongwe, Wilaya ya Kati Unguja leo. Wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk. Idriss Muslim Hija, Waziri  wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban, Mbunge wa Jimbo la Uzini Mohamed Seif Khatib na Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZEC), Hassan Ali Mbarouk.
Baadhi ya wananchi na wazee wa Vijiji vya Jimbo la Uzini wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Umeme Kijiji cha Dongongwe, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja leo, uzinduzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein leo asubuhi.
Baadhi ya wananchi na wazee wa Vijiji vya Jimbo la Uzini wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake katika hafla ya uzinduzi wa Umeme, Kijiji cha Dongongwe, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini, Unguja leo.
Akinamama waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa Umeme, Kijiji cha Dongongwe, Wilaya ya Kati, Jimbo la Uzini, Mkoa wa Kusini, Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake katika hafla ya uzinduzi wa Umeme Kijiji hapo leo.
Meneja wa Shirika la Umeme (ZECO), Hassan Ali Mbarouk alipokuwa akisoma Risala ya Shirika hilo, mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa uzinduzi wa Umeme katika Kijiji cha Dongongwe, Wilaya ya Kati, Jimbo la Uzini, Mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika leo. 

No comments:

Post a Comment