TANGAZO


Monday, December 1, 2014

UN:Ebola bado ni tisho kubwa duniani

Tony Banbury, mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kupambana na Ebola Afrika Magharibi.
Mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kukabiliana na ugonjwa wa Ebola huko Afrika Magharibi, Tony Banbury, amesema ugonjwa huo bado unaweza kuendelea kusambaa duniani.
Mwezi Oktoba, Bwana Banbury aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba iwapo ugonjwa huo utaweza kudhibitiwa, kufikia mwezi Desemba, asilimia sabini ya wagonjwa wa Ebola lazima wawe katika vituo vya tiba, na asilimia sabini ya maiti za waathirika wa Ebola zizikwe kwa usalama.
Katika mahojiano na BBC kwenye mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown, Bwana Banbury mara kwa mara amekataa kuthibitisha kama malengo haya yamefikiwa.
Wafanyakazi wa kuhudumia wagonjwa wa Ebola
Banbury anasema katika wilaya sitini na mbili katika mataifa ya Afrika Magharibi yaliyoathirika zaidi, uwiano wa wagonjwa wa Ebola katika vituo vya tiba na uwiano wa mazishi salama ulikuwa zaidi ya asilimia sabini.
Mkuu huyo ameelezea shauku ya kufikia malengo makubwa na kusema yataweza kufikiwa. Bwana Banbury amethibitisha kuwa Umoja wa Mataifa umedhamiria kuutokomeza ugonjwa wa Ebola miongoni mwa binadamu.

No comments:

Post a Comment