TANGAZO


Monday, December 1, 2014

Uamuzi wasubiriwa kuhusu rufaa ya Lubanga ICC

Mahakama ya ICC inasikiliza rufaa iliyowasilishwa mahakamani na Lubanga akipinga hukumu dhidi yake
Mahakama ya kimataifa ya ICC mjini Hague inatarajiwa kutangaza uamuzi wake leo kuhusu rufaa iliyowasilishwa mahakani katika kesi ya mtu wa kwanza kuhukumiwa na mahakama hio.
Kiongozi huyo wa waasi ,Thomas Lubanga,amepinga hukumu dhidi yake baada ya kupatikana na hatia ya kuwatumia watoto kama wanajeshi ambapo alihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela.
Viongozi wa mashitaka wanasema vijana wenye umri wa miaka 11 walitekwa nyara wakati wa vita vilivyokuwa vinaongozwa na Lubanga zaidi ya miaka kumi iliyopita Mashariki mwa Congo.
Watoto wa kike walitumiwa kama watumwa wa ngono. Hata hivyo wakosoaji wa mahakama hio wameituhumu kwa mwendo wake wa polepole kuhusiana na kesi hio.

No comments:

Post a Comment