TANGAZO


Monday, December 1, 2014

Majina ya kiarabu yaenziwa Uingereza

Zamani jina Oliver ndilo lilikuwa linapendwa sana Uingereza lakini mambo yamebadilika
Utafiti nchini Uingereza Umeonyesha kuwa mwaka huu jina Muhammad ndilo limekuwa maarufu sana linalopewa watoto wavulana na kusukuma jina la Oliver hadi katika nafasi ya pili.
Utafiti huo unaonyesha lionyesha kuwa wazazi wengi wamekuwa wakiwapa wana wao majina ya kiarabu, huku jina la kike Maryam likipendwa sana.
Ni la kwanza kati ya mjina 100 yanayopendwa na wazazi kuwapa watoto wao wasichana. Jina Nur limeshika nafasi ya pili miongoni mwa watoto wa kike.
Kwa watoto wasichana, jina Maryam ndilo linapendwa sana
Majina mengine Omar, Ali na Ibrahim ni miongoni mwa mjina 100 yanayopendwa na kupewa watoto wavulana.
Majina yaliyokuwa yakienziwa sana zamani ya kiingezera na yanayohusishwa na familia ya kifalme, yote yameshuka ngazi na wala hayapendwi sana.

No comments:

Post a Comment