Ofisa mwongoza
ndege wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Bi. Mossy Kitangita akiwahamasisha baadhi ya vijana
na wanafunzi waliotembelea banda la maonesho la kitengo cha kuongozea ndege (hawapo
pichani) kusoma masomo ya Sayansi ili waweze kupata fursa ya kujiunga na fani ya
uongozaji wa ndege ndani na nje ya nchi. (Picha zote na Aron Msigwa - MAELEZO)
Ofisa mwongoza
ndege wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Bi. Mossy Kitangita (kulia) akimweleza Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka namna kitengo cha uongozaji wa ndege katika
uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kinavyofanya kazi na changamoto
wanazokabiliana nazo.
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka (Kushoto) akimuuliza swali Bw.
Nyello Abeid, mkufunzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga nchini kuhusu alipotembelea banda la maonesho la chuo hicho leo
jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya Usafiri wa anga duniani
yanayoendelea nchini.
Meneja wa
Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA) Bw. John Mayunga akifafanua utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya Hali ya
Hewa katika usafiri wa anga.
Mkuu wa
masuala ya Ulinzi na Usalama katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere Bw. Ole Laputi (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wananchi
waliotembelea banda la maonesho la idara hiyo kuhusu baadhi ya vimiminika
visivyoruhusiwa kwa abiria wanaotumia usafiri wa anga.
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka (Kushoto) akitembelea banda la maonesho
la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kuona utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu
na viwanja vya ndege katika maeneo
mbalimbali nchini.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) Bw. Charles Chacha akiongea
na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama wa anga Tanzania na namna
Tanzania ilivyofanikiwa kupunguza idadi ya ajali za ndege.
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya miaka 70 ya Usafiri wa
anga duniani yanayoendelea nchini na namna Serikali kupitia Mamlaka ya Anga
Tanzania (TCAA) ilivyojipanga kuhakikisha usalama wa ndege na abiria wanaotumia
anga la Tanzania.
No comments:
Post a Comment