TANGAZO


Wednesday, December 3, 2014

Diwani wa Kata ya Vijibweni (CCM) atoa Pikipiki mbili kwa ajili ya kusaidia Uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa

Diwani wa Kata ya Vijibweni, Suleiman Mathew (wa tatu kushoto), akimkabidhi ufunguo wa moja kati ya pikipiki mbili, Katibu  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata hiyo, Salum Kabenza Dar es Salaam leo, alizozitoa kwa ajili ya kusaidia uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa katika kata hiyo ambao unatarajiwa kufanyika Disemba 14, 2014.
Wanachama wa CCM wa Kata ya Vijibweni wakiwa kwenye hafla hiyo ya makabidhiano ambayo ilikwenda sanjari na kuhamasishana kuhusu uchaguzi huo.
Diwani wa Kata ya Vijibweni, Suleiman Mathew, akihutubia katika mkutano huo.
Diwani Mathew, akimkabidhi sh. 50,000 Katibu wa CCM, Tawi la Mkwajuni, Shaban Dololo kwa ajili ya kusaidia huduma mbalimbali katika Ofisi yake.
Diwani Mathew akimkabidhi sh. 50,000 Katibu wa CCM, Tawi la Upendo, Beatrice Bwana kwa ajili ya kusaidia kununulia vifaa vya Ofisi kama karatasi na huduma nyingine za ofisini kwake.
Wanachama wa CCM wa Kata hiyo, wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye mkutano huo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment