Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali
ombi hilo la kujiuzulu.
Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema
amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya
Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi
wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
16 Desemba, 2014
No comments:
Post a Comment