Meneja wa TANROADS mkoa
wa Dar es salaam Muhandisi J. Nyamukama akiteta jambo na baadhi ya wahandisi wa
ofisi yake leo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara ya
mkoa wa Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya
Temeke, Bi. Sophia Mjema (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw. Raymond Mushi
wakifuatilia mkutano wa wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam
leo, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Mecki Sadiki akifungua mkutano wa Wajumbe wa Baodi ya Barabara ya
Mkoa wa Dar es Salaam leo. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Theresia
Mmbando na kulia ni Naibu Waziri wa Kazi, Mh. Makongoro Mahanga.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia masuala mbalimbali mada wakati wa mkutano huo.
Makamu Mwenyekiti wa
Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam, Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mh. Mussa Zungu, akichangia kuhusu
hali ya usafi na uimarishaji wa miundombinu katika jiji la Dar es Salaam.
Mmoja wa wajumbe wakichangia mada wakati wa mkutano huo.
Mbunge wa Ubungo Mh. John Myika akichangia
kuhusu hali ya usafi na uimarishaji wa miundombinu katika jiji la Dar es Salaam.
Na Aron Msigwa –
MAELEZO.
16/12/2014. Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki amewataka wahandisi wanaosimamia ujenzi wa miradi ya
barabara katika jiji la Dar es Salaam kuhakikisha kuwa wanawasimamia ipasavyo
wakandarasi wanaojenga miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa viwango na muda uliopangwa
na kuwaondolea wananchi adha ya usafiri inayotokana na ubovu wa barabara.
Aidha,amezitaka Mamlaka
zinazohusika na utoaji wa vibali vya ujenzi katika maeneo mbalimbali katika
jiji la Dar es Salaam kuwachukulia hatua za kisheria wananchi wanaovunja sheria
kwa kujenga majengo na kuta katika maeneo yasiyoruhusiwa na kuziba mifereji ya
maji na
kubomoa kingo za mito hali inayosababisha mafuriko katika makazi ya watu
wakati wa msimu wa mvua.
Akifungua kikao cha
kwanza cha wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam kilichofanyika
leo jijini Dar es Salaam kujadili na kutathmini utekelezaji wa miradi ya barabara kwa mwaka 2014/2015 Bw.
Sadiki amesema kuwa maeneo mbalimbali ya
jiji la Dar es Salaam yamekuwa yakikumbwa na mafuriko kutokana na ujenzi holela katika mikondo ya
maji, uharibifu wa kingo za mito, na uzibaji wa mifereji unaofanywa na baadhi
ya watu kwa kujenga kuta jambo linalosababisha
uharibifu wa miundombinu kutokana na mafuriko wakati wa mvua.
Amesema
kuwa katika
kukabiliana na changamoto za miundombinu ya barabara katika jiji la Dar
es Salaam, zaidi ya shilingi bilioni 88 zimependekezwa kuidhinishwa katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 kwa lengo
la kufanya ukarabati wa kawaida, matengenezo ya barabara za zamani na mpya kwa
kiwango cha lami na ujenzi madaraja
mapya na yale yaliyoharibiwa wakati wa msimu uliopita wa mvua.
Kwa upande wao baadhi
ya wajumbe wa Bodi hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti wameipongeza Serikali
kwa kuendelea kuboresha miundombinu iliyoharibiwa vibaya wakati wa msimu wa
mvua uliopita maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, ujenzi wa barabara ya Uhuru,Daraja la
Kinyerezi, Ujenzi wa kituo cha mabasi eneo la Machinga Complex, utekelezaji wa
mradi wa barabara ya Shingofeni, Barabara ya Mombasa –Moshi Bar na ujenzi wa
barabara ya Ulongoni A kuelekea Kilimani.
Wamesema
kuwa juhudi za
usafi wa mito, madaraja na mifereji katika maeneo mbalimbali ya jiji la
Dar es Salaam lazima iwe shirikishi ili mafanikio ya kuliweka jiji
katika hali ya
usafi na usalama wakati wa msimu wa mvua yaweze kuonekana na kuwaondolea
usumbufu wananchi.
No comments:
Post a Comment