TANGAZO


Friday, December 5, 2014

Maadhimisho ya Wiki ya Usafiri wa Anga yafikia kilele chake leo jijini Dar es Salaam

Wadau mbalimbali wakishiriki sherehe za kilele cha Wiki ya Usafiri wa Anga zilizofanyika leo katika viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga jijini Dar es Salaam.
 Meneja mradi  wa ujenzi wa  jingo jipya la abiria (Terminal 3) katika uwanja wa ndege  wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Muhandisi Mbaraka Shafii akimweleza Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kulia) maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo utakaokuwa na uwezo wa kuwahudumia abiria milioni 6 kwa mwaka.
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akimweleza jambo Muhandisi Mwanaidi Mkwizu kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mh. Peter Selukamba.
 Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Bw.Ralph Goetz, Mtaalam wa masuala ya Miundombinu  wa kampuni ya Switzport  Tanzania kuhusu ujenzi wa jengo la kutolea huduma kwa abiria wa kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa sekta binafsi katika kuendeleza  sekta ya usafiri wa anga nchini.  
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kulia) akiwasisitiza baadhi ya wahandisi wa wanawake wanaosimamia mradi wa ujenzi wa jengo jipy la abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa. 
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea maandamano ya wadau wa sekta ya Usafiri wa Anga walioshiriki maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Usafiri wa Anga leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa Sekta ya Usafiri wa Anga wakishiriki maandamano wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Usafiri wa Anga jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga kilichoko jijini Dar es salaam wakipita mbele ya mgeni rasmi, Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa kilele cha Wiki ya Usafiri wa Anga leo jijini Dar es Salaam.  
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mh. Peter Serukamba wakifurahia jambo walipotembelea banda la maonesho la kitengo cha kuongozea ndege katika uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akipata maelezo kutoka kwa mkuu wa kitengo cha Zimamoto na Uokoaji  uwanja wa ndege, Sajenti Thomas Lichenjela alipotembelea banda la maonesho la kitengo hicho kuona namna walivyojipanga kukabiliana na majanga mbalimbali. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mafunzo kwa marubani Tanzania Bw. Quentin Gray (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na watendaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania namna kituo chake kilivyojipanga kutoa mafunzo katika fani ya urubani na uongozaji wa ndege leo jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Wiki ya Usafiri wa Anga.
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akiwapokea baadhi ya wanafunzi wa shule za 3 msingi kutoka wilaya za Temeke, Kinondoni na Ilala walioshiriki ziara ya mafunzo katika masuala ya Anga katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar. Vijana hao pia walifanya ziara katika uwanja wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere. 
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe, Viongozi na wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mh. Peter Serukamba na Viongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule za 3 msingi kutoka wilaya za Temeke, Kinondoni na Ilala walioshiriki ziara ya mafunzo katika masuala ya Anga katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar. (Picha zote na Aron Msigwa – MAELEZO)

No comments:

Post a Comment