TANGAZO


Friday, December 5, 2014

Wafanyakazi wa TBL waliopima virusi vya ukimwi wazawadiwa zawadi mbalimbali

Mgeni rasmi Ofisa Uendeshaji, Rasirimali watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Collins Constantine, akishishirikiana na wafanyakazi wenzake wa TBL kuwasha mishumaa kuwakumbuka wenzao waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa Ukimwi.
 Mgeni rasmi, Ofisa Uendeshaji, Rasirimali watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Collins Constantine akikabidhi zawadi ya jiko la gesi kwa Christopher Mchome, baada ya kushinda bahati nasibu ya wafanyakazi waliopima afya zao, wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi, Dar es Salaam juzi.
Mchome akisaidiwa na wenzake kubeba jiko baada ya kushinda bahati nasibu ya wafanyakazi wa TBL.
Wasanii wakitoa burudani ya michezo mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo ya Siku ya Ukimwi kwa wafanyakazi wa TBL.
Wafanyakazi wa TBL wakisubiri kwa shauku kubwa zawadi zilizotolewa na kampuni hiyo ili zichezeshwe bahati nasibu kwa wafanyakazi waliopima afya zao kwa hiari.
Wakiwa na shauku ya kupata zawadi, wafanyakazi wa TBL wakipata kinywaji huku wakisubiri bahati nasibu iliyoandaliwa na kampuni hiyo, wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi.

Mfanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL, Joel Saganya akiwa mwenye furaha baada ya kushinda godoro.
 Wasanii wakionyesha umahiri wao wa kucheza Sarakasi. Sarakasi 
ilikuwa moja ya michezo iliyowavutia wafanyakazi wa TBL
Wakiwa na shauku ya kupata zawadi, wafanyakazi wa TBL wakipata kinywaji huku wakisubiri bahati nasibu iliyoandaliwa na kampuni hiyo, wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi.

No comments:

Post a Comment