Baadhi ya wataalam wa sekta na waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao maandalizi ya kongamano la kimataifa la kinga ya jamii litakaofanyika jijini Arusha kuanzia Disemba 15 hadi 17 mwaka huu.
Baadhi ya wataalam wa sekta na waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao maandalizi ya kongamano la kimataifa la kinga ya jamii litakaofanyika jijini Arusha kuanzia Disemba 15 hadi 17 mwaka huu. (Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO)
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO
05/12/2014
Serikali ya Tanzania
kupitia Wizara ya Fedha, Idara ya Kuondoa Umaskini inaandaa kongamano la
kimataifa linalohusu kinga ya jamii litakaofanyika jijini Arusha kuanzia
Disemba 15 hadi 17 mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo
jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile
wakati wa kikao cha wataalam wa sekta na waandishi wa habari kuhusu kongamano
hilo.
Dkt. Likwelile alisema
kuwa Mgeni Rasmi atakayefungua kongamano hilo anatarajiwa kuwa Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na unatarajiwa
kufungwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Kongamano hilo litahusisha
watunga sera, watafiti na watu wanaojihusisha moja kwa moja kwenye kubuni, kupanga na kutekeleza programu
za kinga ya jamii na mifumo yake kwa kwa lengo la kubadilishana ujuzi na
uzoefu.
Dkt. Likwelile alisema
kuwa majadiliano katika kongamano hilo la siku tatu yatalega kuwajengea
washiriki uelewa zaidi juu ya kinga ya jamii na matumizi yake kwa sera,
programu na utawala pamoja na kushirikiana katika kutumia matokeo ya tafiti,
masuala ya kujifunza na namna bora ya kuandaa na kutekeleza programu na mifumo
inayohusu kinga ya jamii.
Malengo mengine ya kongamano
hilo ni pamoja na kuainisha mambo ya msingi yanayohusu kinga ya jamii ambayo
yanahitaji kuchukuliwa na kuingizwa kwenye agenda kuu ya kinga ya jamiii kwa
ajili ya maendeleo ya usoni na kuandaa uwanja wa kubadilishana uzoefu na
hatimaye kuwa na mikakati mizuri ya pamoja inayohusu kinga ya jamii.
Nchi zitakazoshiriki
kongamano hilo linaloandaliwa na Serilkali ya Tanzania kwa kushirikiana na
UNICEF, ILO, UNAIDS NA EPRI ni Kenya, Uganda, Bangladesh, Afghanistan,Msumbiji,
Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na
mwenyeji Tanzania.
No comments:
Post a Comment