Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Theresa Mghanga (aliyesimama) akiongea katika mkutano kati ya Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi na watumishi wa Wizara hiyo.
Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Maimuna Tarishi (hayupo pichani) leo (Alhamisi, Nov. 20, 2014).
Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Maimuna Tarishi (hayupo pichani) leo (Alhamisi, Nov. 20, 2014).
Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Maimuna Tarishi (hayupo pichani) leo Alhamisi, Nov. 20, 2014. (Picha zote na Said Benjamin)
Na Mwandishi Wetu
Watumishi wa Wizara ya
Katiba na Sheria wameaswa kuendeleza ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu
yao ili kutimiza malengo ambayo Wizara imejiwekea.
Akizungumza na watumishi wa
makao makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Novemba 20, 2014), Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi amesema ushirikiano na upendo
ni ngunzo muhimu za mafanikio katika taasisi yoyote.
“Watumishi wa umma, hasa
tuliopo Dar es Salaam, tunatumia muda mrefu tukiwa kazini hivyo tunatakiwa
tupendane na tushirikiane katika kutekeleza majukumu yetu kama timu moja,”
amesema Bi. Tarishi.
Katibu Mkuu huyo alikuwa
alikuwa akizungumza na watumishi hao kwa mara ya kwanza tangu alipohamishiwa
Wizarani hapo hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kutoka Wizara ya Mali Asili
na Utalii ambako alikuwa Katibu Mkuu.
Aliongeza: “Tufanye kazi kwa
malengo na kasi… tujiulize, wiki hii nimefanya nini, nimetekeleza nini,”
alisema kiongozi huyo na kusisitiza kuwa watumishi wa Wizara ya Katiba
wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Wizara.
Akizungumza katika mkutano
huo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Wizara hiyo Bi. Theresa Mghanga
alimshukuru Katibu Mkuu kwa kutenga muda kukutana na watumishi na kusisitiza
umuhimu wa watumishi wote wa Wizara kuzingatia sheria, kanuni na miongozo
katika utumishi wao.
“Tuwahi kazini na kutimiza
wajibu wetu na tujione kuwa tuna deni kwa nchi yetu,” alisema Bi. Theresa
katika mkutano huo uliohudhuriwa na Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na
watumishi wote wa Wizara waliopo makao makuu.
No comments:
Post a Comment