Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Titus Kamani, akimpongeza Mkurugenzi Mtendai wa Covenant Bank. Bibi Sabetha Mwambenja kwa benki yake kuwa benki ya kwanza kutoa mikopo ya ng’ombe 83 kwa wafugaji nchini, Mkurugenzi huyo alimtembelea Mh. Waziri ofisini kwake kuitikia wito ili kujadiliana namna ambavyo benki hiyo invyoweza kuwafikia wafugaji wengi zaidi.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Titus Kamani, akimpongeza Mkurugenzi Mtendai wa Covenant Bank. Bibi Sabetha Mwambenja kwa benki yake kuwa benki ya kwanza kutoa mikopo ya ng’ombe 83 kwa wafugaji nchini, Mkurugenzi huyo alimtembelea Mh. Waziri ofisini kwake kuitikia wito ili kujadiliana namna ambavyo benki hiyo invyoweza kuwafikia wafugaji wengi zaidi.
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam 20 Nov 2014
WAZIRI wa Maendeleo
ya Mifugo na Uvuvi Dr. Titus Kamani, ameipongeza Covenant Bank kwa kuwa
mkombozi kwa wafugaji kwa kuwapatia mikopo ya ng’ombe wa maziwa, suala ambalo
limekuwa gumu kwa taasisi nyingi za kifedha.
Waziri kamani
ameyasema hayo wakati alipotembelewa na ujumbe wa benki hiyo Ofisini kwake
jijii Dar es Salaam katika kujadili njia bora zaidi ambazo Benki hiyo inaweza
kuzitumia kwa kuwafikia wafugaji wengi zaidi.
“Ninawapongeza sana
kwa namna ambavyo mmeanza kwa kuwa mfano wa kuwawezesha, Wafugaji wadogo ambao
kwa muda mrefu taasisi za kifedha zimekuwa mbali nao, Wengi wamekuwa hawana
Uwezo wa kukopesheka kutokana na kutokuwa na mfumo Rasmi wa kutambulika katika
taasisi hizo” alisema Kamani na Kuongeza.
Nimewaita hapa nikiwa
na wito kwenu, kuwataka muangalie namna ya kuendelea kuwawezesha wafugaji wengi
zaidi, ndani na nje ya Dar es Salaam, Tunashukuru mmeanza na Ng’ombe wa Maziwa lakini
kuna fursa nyingine kwa wafugaji wa ng’ombe wa nyama huku kuna utajiri Mkubwa
sana na inaweza kuchangia pato la taifa kwa kiasi kikubwa.
Dk. Kamani aliongeza
kwa kutoa wito kwa taasisi za kifedha kama Covenant Bank kuendeleza ubunifu wa
utoaji wa mikopo kwa kulingana na mazingira halisi ya uwekezaji, Huku akiahidi
kuwa serikali itaendelea kuunga mkono jitihada za benki hiyo katika kuwakomboa
wafugaji.
Akijibu hoja za Mh.
Waziri Mkurugenzi Mtendaji wa Banki hiyo Bibi. Sabetha Mwambenja amesema kuwa,
Anashukuru kwa namna ambavyo serikali imeupokea mradi huo na kuunga mkono na
kuahidi kuendelea kubuni miradi ambayo itawakomboa Watanzania hasa
wajasiriamali wadogo wasio katika sekta Rasmi.
“Ninashukuru kwa
namna Serikali ambavyo imeupokea mradi huu, na kuupa kipaumbele kikubwa, tunawaahidi
kuendelea kutekeleza miradi mingine ya kipekee itakayo wezesha Watanzania wasio
katika sekta Rasmi kumiliki nyenzo muhimu za kujiongezea kipato kwani hawa ndio
wanamchango mkubwa katika ukuaji wa Uchumi.
Aidha mkurugenzi huyo
alitanabaisha kuwa wataendelea kuwawezesha wajasiriamali wadogo ikiwemo
wafugaji kutokana na fursa zilizopo na kuhakikisha wanakuwa wa kwanza katika
kubuni na kuanzisha huduma za kipekee kwa Watanzania.
Siku
chache zilizopita Covenant Bank ilitoa mikopo ya Ng'ombe 83 kwa kikundi cha
wafugaji wadogo cha Somangira waliopo Kigamboni Wilaya ya Temeke, Jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment