Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dimani Mkoa wa Magharibi CCM katika viwanja vya Ofisi ya Mkoa Amani leo alipofika kuzungumza na Mabalozi na wenyeviti wa maskani katika mfululizo waziara zake za kuimarisha Chama Mikoa ya Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akitia saini kitabu cha wageni katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa Amani alipohudhuria katika mkutano wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dimani Mkoa wa Magharibi CCM uliowashirikisha Mabalozi na wenyeviti wa maskani katika mfululizo waziara zake za kuimarisha Chama Mikoa ya Unguja.
Mabalozi wa Jimbo la Magogoni wakinyoosha mikono juu kushagilia wakati walipotamulishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya ya Dimani katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama katikaMikoaya Unguja.
Wajumbe wa Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya ya Dimani kutoka Jimbo la Magogoni wakifuatilia kwa makini taratibu za Mkutano huo zilizotumika kwa Viongozi wakuu wa CCM walipozungumzia masuala mbali mbali katika ziara ya kuimarisha Chama iliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani.
Wajumbe wa Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya ya Dimani kutoka Jimbo la Fuoni wakifuatilia kwa makini taratibu za Mkutano huo zilizotumika kwa Viongozi wakuu wa CCM walipozungumzia masuala mbali mbali katika ziara ya kuimarisha Chama iliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiwa kwenye meza kuu pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, visiwani Zanzibar, Vuai Ali Vuai (kulia), wakati Dk. Shein, alipokuwa katika Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya ya Dimani, ukumbi wa CCM Mkoa Amani mjini Unguja leo.
Katibu Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Dimani Mkoa wa Magharibi Kichama alipokuwa akihamasisha Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya hiyo walipokuwa katika Mkutano maalum uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Sheinkatika ziara zake za kuimarisha Chama katika Mikoa ya Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea risala ya mabalozi iliyosomwa na Balozi Kasim Hassan Haji katika Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya ya Dimani katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama katika Mikoaya Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wanachi na Wanachama wa CCM katika Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya ya Dimani katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama katikaMikoaya Unguja. |
Na Said Ameir, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewakumbusha viongozi
waliochaguliwa kupitia Chama cha Mapinduzi kuwa wanawajibu kushirikiana na wanachama
wenzao kukiimarisha chama hicho katika kila ngazi.
“Viongozi hawa (wabunge
na wawakilishi)tumewapitisha katika vikao vyetu na kuchaguliwa na wananchi
hivyo wana wajibu wa kuendelea kukitumikia chama na kwa umoja wetu kushirikiana
kukijenga na kukiimarisha kwa nguvu zetu sote” Dk. Shein amesema.
Dk. Shein ametoa wito
huo leo wakati alipokuwa akizungumza na mabalozi wa nyumba kumi na wenyeviti wa
maskani za chama hicho wa wilaya ya kichama ya Dimani mkoa wa kichama wa
Magharibi, Unguja katika mfululizo wa mikutano yake na viongozi hao katika wilaya
za Unguja na Pemba.
Alisema kuwa viongozi
hao wanapaswa pia kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo katika maeneo
yao ikiwemo kuchangia miradi ya maendeleo na shughuli nyingine za wananchi na wanapaswa
kuwapimwa kwa kuzingatia ufanisi na ushiriki wao katika shughuli hizo.
Dk. Shein aliwaambia viongozi
hao kuwa lengo la mikutano hiyo ni kuimarisha chama hicho kwa kuzungumzia mambo
muhimu yeye mustakabala wa Chama cha Mapinduzi na maedeleo ya Zanzibar.
Kwa hivyo aliwataka
viongozi katika ngazi mbali mbali za uongozi kuitisha vikao kama Katiba ya
chama hicho inavyoelekeza kuzungumzia masuala yote ya maendeleo ya chama hicho
pamoja na kushughulikia hitilafu zinapotokea miongoni mwa viongozi na wanachama.
“Hitilafu zinapotokea
baina yetu zizungumzwe katika vikao vyetu ili tuelewane na kamwe tusipuuze
utaratibu wa chama chetu wa kukosoana vinginevyo tutakuwa tunakaribisha majungu
ambayo hayakisadii chama chetu” Dk. Shein aliwaeleza viongozi hao.
Katika mkutano huo,
Dk. Shein alitoa wito pia wa kuimarishwa kwa matawi na maskani za chama hicho
kwa ajili ya kukipa nguvu na kuongeza kasi zaidi ya utekelezaji wa shughuli za
chama ikiwemo kushinda chaguzi zijazo.
Aliwataka wana CCM na
wananchi wa Zanzibar kuendelea kuenzi M uungano wa Zanzibar na Tanganyika ambao
ulizaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo sasa imetimiza miaka 50 kwa
mafanikio makubwa.
“Muungano ni uamuzi
sahihi uliofanywa na viongozi wetu waasisi ... ni uamuzi ambao ulifanywa
hadharani kwa kushirikisha Baraza la Mapinduzi kwa upande Zanzibar na kwa Tanganyika
lilihusika Baraza la Mawaziri” Dk. Shein alieleza na kusisitiza kuwa kuimarisha
Muungano ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Aliongeza kuwa
kuimarisha Muungano ndio kuenzi Mapinduzi ya mwaka 1964 kwa kuwa bila ya Mapinduzi
hayo hakungekuwa na Muungano hivyo wananchi wa Zanzibar hawana budi kusimama
kidete kutetea Muungano kwa nguvu zao zote.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa
na viongozi mbali mbali wa chama hicho wakiwemo wajumbe wa Kamati Kuu na
Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho pamoja na baadhi ya mawaziri, Dk. Shein
aliwahakikishia viongozi hao kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali
kushughulikia ahadi zake na pia kuondoa kero mbalimbali zinazowakabili
wananchi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Mkoa wa Magharibi Yussuf Mohamed
alieleza kuwa wananchi wa Mkoa huo wana kila sababu ya kujivunia uongozi wa Dk.
Shein kwa namna ulivyojidhahtiti kutekeleza ahadi na mipango mbali mbali ya
maendeleo na kubadili maisha ya wananchi.
“katika miaka mine ya
uongozi wako tunmeona jitihada zako, ukereketwa wako na uzalendo kuwatumikia
wananchi na kuwaletea maendeleo” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa jitihada
hizo zimebadili maisha kila ya mwananchi.
Naye
Nibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai,
akimkaribisha Dk. Shein kuzungumza na viongozi hao, alieleza kuwa chama hicho
kimezidi kuimarika tangu uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo kimeweza kushinda katika
baadhi ya chaguzi ndogo zilizofanyika na kueleza kuwa kimekuwa kikionesha
uungwana kwa kukubali matokeo pale kinaposhindwa badala ya kulalamika kama vinavyofanya
vyama vingine.
Aidha, alihimiza
utangazaji wa mafanikio mbalimbali za utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya
nchi ili wananchi waweze kuelewa hatua zinazochukuliwa na serikali yao kuwaletea
maendeleo.
No comments:
Post a Comment