Mfichua siri kuhusu tuhuma za rushwa kutolewa na Qatar ili kuiwezesha nchi hiyo kushinda nafasi ya kuandaa Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022 ameiambia BBC kuwa anaishi kwa hofu kutokana na hatua yake hiyo.
Mwaka 2011, Phaedra al-Majid alidai kuwa maafisa wa Qatar walijitolea kuwalipa maafisa watatu wa vyama vya soka barani Afrika kiasi cha dola milioni moja na nusu ili kuiunga mkono Qatar kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa duniani.
Baadaye Bi Phaedra al-Majid aliondoa tuhuma hizo, lakini sasa anasema alilazimishwa kubadili kauli yake. Anasema ameingia katika hali ya uendawazimu ya "kujiona anaonewa kila wakati, hofu na vitisho" (na kwamba atajiona mkosaji maisha yake yote.)
Kamati ya Qatar ya uandaaji wa Fainali za Kombe la Dunia imesema ushahidi wa Phaedra al-Majid ulitiliwa mashaka na timu ya uchunguzi ya FIFA, na kwamba tuhuma zote zilichunguzwa na kutupiliwa mbali.
No comments:
Post a Comment