Wanafunzi wa Kitivo cha Uhandisi wa Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (COET), Kampasi ya Kijitonyama wakimsikiliza kwa makini mmiliki wa
mtandao wa Popote Media, Gillbart Mlaseko (kushoto), alipokuwa akiwafafanulia
jambo kuhusu shindano la AppStar linaloendeshwa na Vodacom
Tanzania linalohusu ubunifu wa program za simu za mkononi. Washindi watajishindia
zawadi mbalimbali zikiwemo pesa taslim na safari za kwenda nchini India na
Barcelona kushiriki katika shindano hilo ngazi ya Kimataifa. Wapili kushoto ni
Meneja Uhusoiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Abigail Ambweni.
Mmoja wa wanafunzi wa Kitivo cha Uhandisi cha Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (COET), Kampasi ya Kijitonyama akimuuliza swali mshindi wa
shindano la App Star mwaka 2012, Ernest
Mwalusanya kuhusu na shindano la
AppStar linaloendeshwa na Vodacom Tanzania linalowalenga wabunifu wa program za
simu za mkononi ambapo washindi watajishindia
zawadi mbalimbali, zikiwemo pesa taslim na safari za kwenda nchini India na
Barcelona kushiriki katika shindano hilo katika ngazi ya Kimataifa.
Mshindi wa
shindano la AppStar mwaka 2012 Ernest Mwalusanya, akiwafafanulia
jambo baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Sayansi
ya Kompyuta kuhusu jinsi ya kushiriki katika shindano la AppStar, linaloendeshwa na Vodacom
Tanzania. Shindandano hilo ni mahususi
kwa wataalamu wabunifu wa kutengeneza mobile applications. Washindi watajishindia
zawadi mbalimbali, zikiwemo pesa taslim na safari za kwenda nchini India na
Barcelona kushiriki katika shindano la ngazi ya Kimataifa. (Picha zote na mpigapicha wetu)
No comments:
Post a Comment