TANGAZO


Friday, November 28, 2014

Rais Jakaya Kikwete kurejea nchini kesho mchana

Rais Kikwete, alipokuwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Marekani, akianza kazi nyepesi nyepesi baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume kwenye hospitali hiyo.
Rais Kikwete, akitoka katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Marekani, akisindikizwa na Daktari aliyemfanyia upasuaji wa tezi dume baada ya kupata nafuu.
Rais Kikwete, akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Mula Mula na baadhi ya Maofisa wa ubalozi huo, walipomtembelea kumjulia hali alipokuwa hotelini wakati akiendelea kujiuguza jeraha la upasuaji wa tezi dume.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atarejea nchini kesho mchana, Jumamosi, Novemba 29, 2014 kutoka kwenye matibabu nchini Marekani.

Mhe. Rais atawasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar Es Salaam, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates saa 9:20 mchana.

Tunakaribisha vyombo vya habari kuwepo Uwanjani kwa ajili ya ujio wa Mhe. Rais. Tunashauri tuwe tumefika Uwanjani saa 8:30 mchana.


ASANTENI


IMETOLEWA NA:

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS,

IKULU – DAR ES SALAAM.

28 NOVEMBA,2014

No comments:

Post a Comment