Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard (katika), akimfafanulia jambo kuhusiana na simu aina ya Vodafone smart kicka Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema(kulia) alipofika kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Mbagala zakiemu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Shophia Mjema akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Mbagala zakiemu jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika leo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Shophia Mjema(kulia)akiongea na Hajira Said ambaye alikuwa mteja wa kwanza kufika katika duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Mbagala zakiemu jijini Dar es Salaam mara baada ya Mkuu wa wilaya hiyo kulizindua.
Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard (kushoto) na Matina Nkurlu Meneja uhusiano wa kampuni hiyo (katikati) wakimsikiliza jambo kwa umakini Mkuu wa Wilaya ya Temeke Shophia Mjema (kulia) mara baada ya kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Mbagala zakiemu jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Shophia Mjema wane toka kulia akiwa kwenye picha ya
pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania mara baada ya kuzindua duka
jipya la kampuni hiyo lililopo Mbagala zakiemu jijini Dar es Salaam leo.
MKUU wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema ametoa ushauri kwa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kufungua zaidi vituo
vya kutoa huduma kwa wateja wilayani humo ili kuwawezesha wateja wake
kupata huduma kwa karibu badala ya kuzifuata mbali na kupoteza muda
mwingi ambao wangeutumia kufanya shughuli za uzalishaji.Alitoa ushauri
huo wakati akifungua duka la Vodacom la Mbagala ambapo pia alitoa
pongezi kwa hatua hiyo.
Katika
kuhakikisha wakazi wa vitongoji vya Mbagala na maeneo jirani ya
Mtoni,Temeke na Tandika wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom leo imefungua duka jipya katika eneo la Mbagala
Zakiemu.
Mbagala
ni moja ya kitongoji maarufu katika cha jiji la Dar es Salaam ambacho
kinakuwa kwa kasi kwa maendeleo na kuwa kivutio cha wawekezaji wengi
kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu na shughuli mbalimbali za
kibiashara ikiwemo kituo kikubwa cha mabasi yanayoelekea mikoa ya Kusini
ya Lindi na Mtwara.
Duka
hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma
mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma kwa mawakala wa Mpesa
na uuzaji wa bidhaa za Vodacom na litawawezesha wateja wa Mbagala na
vitongoji vyake wakiwemo wasafiri wanaoelekea mikoa ya Kusini na
wateja kutoka maeneo ya Temeke,Kurasini,Mtoni na Tandika.Mtandao wa
Vodacom unaongoza kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika
wilaya ya Temeke.
Hassan
Saleh Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Vodacom Tanzania,alisema
ufunguzi wa duka hili la kisasa ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom
kuendeleza kuboresha maisha murua kwa kila mtanzania kwa kupata huduma
za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote
pale walipo ikiwemo huduma mpya ya kilimo klabu inayolenga kuwawezesha
wakulima nchini.
“Uzoefu
na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao
unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya
juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya
wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua
maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na
ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia na
tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na tunawakaribisha
ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata huduma bora
kwa gharama nafuu.”Anasema Saleh.
Vodacom
ina mtandao wa maduka 84 nchi nzima na wakala mbalimbali wakuuza
bidhaa zake nchini na duka lililofunguliwa leo ni la 5 kufunguliwa
katika wilaya ya Temeke.
No comments:
Post a Comment