Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif S. Rashidi (Mb)
UFAFANUZI KUHUSU UHABA
WA DAWA MUHIMU NA VIFAA TIBA
Kuna taarifa katika vyombo vya habarii liyotolewa na Shirika
lisilo la Kiserikali la SIKIKA, kwamba serikali haijalipa kiasi cha shilingi
bilioni 90 kwa bohari kuu ya dawa na kusababishia ukosefu dawa katika baadhi ya hospitali.
Ni kweli bohari kuu ya dawa imepungukiwa fedha za kununulia
dawa , lakini sio kwa kiasi cha kushindwa kutoa huduma kabisa kama inavyoelezwa.
Kiasi cha pesa kinachotajwa si kigeni na serikali imekua ikitoa kiasi cha
fedha kidogo kidogo ili kuongeza uwezo wa bohari ya dawa iweze kufanya kazi ya kununua na kusambaza
dawa.
Katika kukabiliana na
hali hii hospitali zote kupitia waganga wakuu wa mikoa na wilaya zimeagizwa
kupeleka asilimia 50 ya mapato
yanayotokana na uchangiaji kwenda bohari kuu ya dawa.
Kuhusu ukosefu wa matibabu katika Taasisi ya Saratani ocean
road, ni kweli kwa sasa baadhi ya
mashine hazifanyi kazi na zinazofanya kazi ni chache hivyo kuzidiwa wakati fulani.
Hatahivyo wizara imekwisha
agiza vifaa hivyo ambavyo ni ghali sana toka Canada na vinategemewa kufika
wakati wowote kuanzia sasa na pia ikumbukwe kuwa matibabu yanatotolewa bila malipo na gharama zote ni za serikali.
Wizara kwa sasa imeagizwa katika mpango wa matokeo makubwa
sasa (BRN)ambapo wataalam wanamalizia kazi za utekelezaji wa mpango huo. Ambapo
pia umezingatia namna ya kukabiliana na
jinsi ya kuhakikisha dawa zinapatikana kwa wakati katika vituo vya matibabu na kuiboresha zaidi bohari ya dawa.
Baada ya kuanza utekelezaji huo suala la ukosefu wa dawa na vifaa tiba utapungua kwa kiasi kikubwa sana.
Pamoja na wizara kupeleka bohari tyadawa pesa kwa ajili ya
ununuzi wa dawa na vifaa tiba, hospitali zihakikishe zinapeleka asilimia 50 ya
mapato kama zilivyoagizwa na kutokufanya hivyo kiongozi husika atawajibishwa.
Mwisho wizara inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba dawa na
vifaa tiba muhimu vinapelekwa katika vituo vyote , pia inaendelea kufanya kazi
na taasisi zote zisizo za kiserikali kwa karibu kwa faida ya wananchi wote.
Imetolewa na :-
Dkt. Seif S. Rashidi (Mb)
WAZIRI WA AFYA NA
USTAWI WA JAMII
27/10/2014
No comments:
Post a Comment