Nembo ya Chama kipya cha ACT Tanzania
Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Mohammed Massaga.
|
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Tanzania, Samson Mwigamba (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo (hawapo pichani), kuhusu maazimio ya mkutano wa tatu wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT Tanzania uliofanyika Oktoba,5, 2014. Kulia ni Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Mohammed Massaga na Katibu wa Ngome ya Vijana wa chama hicho, Philip Mallaki.
Wapiga picha wa vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
KATIBU Mkuu wa Chama cha ACT Tanzania, Samson Mwigamba amesema milango ipo wazi kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto kujiunga na chama hicho iwapo atapenda kufanya hivyo.
Mwigamba ameyasema hayo Dar es Salaam leo asubuhi wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati akitoa maazimio ya mkutano wa tatu wa Kamati Kuu ya Chama cha ATC Tanzania uliofanyika Jumamosi Oktoba 2014 katika Hoteli ya Vina jijini Dar es Salaam.
Alisema Zitto anakaribishwa kujiunga na chama hicho iwapo atapenda kufanya hivyo na sisi yeye tu hata wananchi wengine watakaopenda kufanya hivyo kwani chama hicho licha ya kuwa na miezi michache tangu kuanzishwa kwake kimepata wanachama zaidi 18,000.
"Chama chetu kinamafanikio makubwa na kimekubali na watu wengi hivyo wanaotaka kujiunga tunawakaribisha kwani tunawatu maarufu ambao tayari wamejiunga, " alisema Mwigamba.
Katika hatua nyingine chama hicho kimesikitika na kushindikana kupatikana kwa maridhiano baina ya makundi mbalimbali ya kisiasa nchini kuhusu mchakato wa na maudhui ya Katiba Mpya.
"Kamati kuu imesikitishwa zaidi na uamuzi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake wa kuteka na kuburuza mchakato wa katiba kwa kuegemea matakwa ya sheria bila kujali uhalali mpana wa kisiasa na kijamii nchini.
Alisema mchakato huo wa Bunge la Katiba umeitimishwa kwa mtindo ambao umeacha mgawanyiko na mpasuko mkubwa wa kisiasa na kijamii nchini badala ya kujenga umoja na mshikamano wa kitaifa, ambalo ndilo lengo la msingi la mchakato wenyewe.
Mwigamba alisema maazimio mengine yaliyofikiwa na kamati kuu ni kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), atoe ripoti kuhusu uchunguzi wa wizi wa fedha zinazodaiwa kuwa ni za umma uliofanyika kupitia akaunti ya Escrow iliyotokana na mgogoro baina ya Tanesco na IPTL.
Akizungumzia kuhusu Bodi ya Mikopo kwa Vyuo vikuu, alisema wamesikitishwa na taarifa kuwa zaidi ya wanafunzi 50 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali vya elimu ya juu nchini hawatapata mkopo.
Alisema kamti hiyo haikubaliani na hali hiyo na inawahimiza wanafunzi,vijana na wadau wa elimu nchini kuungana na chama cha ACT Tanzania katika kuishinikiza Serikali kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapatiwa mikopo ili waweze kuipata elimu ya juu ambayo inahitajika sana kwa mustakabali wa nchi.
Mwigamba alihitimisha taarifa yake kwa kusema uzinduzi rasmi wa chama hicho kuwa utafanyika Desemba mwaka huu jijini Dar es Salaam katika eneo litakalopangwa.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment