Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha Rose Migoro (katikati ) akizindua Zahanati kwa ajili ya matibabu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA Nakayama, iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji, mkoani Pwani, wakati mahafali ya pili yaliyofanyika jana. (Picha zote na Magreth Kinabo, Maelezo)
Baadhi ya wahitimu wa Elimu ya Sekondari ya kidato cha nne kutoka katika Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji, mkoani Pwani, wakiwa katika maandamano kwa ajili mahafali ya pili yaliyofanyika jana.
Baadhi ya wake za viongozi wakiwa katika sherehe za mahafali hayo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika mahafali hayo.
Msanii Vicky Kamata akiimba wimbo wa kumpongeza mke wa Rais,Mama Salma Kikwete na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), kwa juhudi zake za kumkomboa mtoto wa kike kielimu wakati mahafali ya pili Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji, mkoani Pwani yaliyofanyika jana.
Wahitimu wa Elimu ya Sekondari ya kidato cha nne kutoka katika Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu ya WAMA, Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji, mkoani Pwani, wakiwa wakimpatia maua mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake wa kusaidia watoto wa kike wakati wa sherehe za mahafali ya pili yaliyofanyika jana.
Msanii Vicky Kamata akiimba wimbo wa kumpongeza mke wa Rais,Mama Salma Kikwete na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), kwa juhudi zake za kumkomboa mtoto wa kike kielimu wakati mahafali ya pili Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu ya WAMA Nakayama, iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji, mkoani Pwani yaliyofanyika jana.
Baadhi ya wahitimu wa Elimu ya Sekondari ya kidato cha nne kutoka katika Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji, mkoani Pwani, wakifurahia na jambo na mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, wakati wa sherehe za mahafali ya pili yaliyofanyika jana.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha Rose Migoro (kulia), akimkabidhi cheti cha kuhitimu Elimu ya Sekondari, mwanafuzi wa kidato cha nne kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu ya WAMA Nakayama, iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji, mkoani Pwani, Ulizeni Ngonyani katika mahafali ya pili yaliyofanyika jana.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migoro (kulia) akimkabidhi cheti Kaimu Balozi wa Japan nchini, Kazuyoshi Matsu naga ikiwa ni ishara ya kutambua msaada wa nchi hiyo wa kuisaidia Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika hatarishi ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji mkoani Pwani wakati wa sherehe ya mahafali ya pili ya shule hiyo yaliyofanyika jana.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migoro (kulia) akimkabidhi cheti Kaimu Balozi wa Japan nchini, Kazuyoshi Matsu naga ikiwa ni ishara ya kutambua msaada wa nchi hiyo wa kuisaidia Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika hatarishi ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji mkoani Pwani wakati wa sherehe ya mahafali ya pili ya shule hiyo yaliyofanyika jana.
Na Magreth Kinabo
WANANCHI wameshauriwa kuisoma Katiba Mpya Inayopendekezwa sura kwa sura na ibara kwa ibara ili waweze kupata uelewa wa masuala mbalimbali yaliyomo ndani ya Katiba hiyo na kuacha kusikiliza maneno ya watu yenye nia ya kupotosha ukweli.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migiro wakati wa sherehe za mahafali ya pili ya Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA Nakayama, iliyopo wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Dkt . Migiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo, ambayo ilihudhuriwa na baadhi ya viongozi , wakiwemo baadhi ya wake za viongozi na wageni wengine mbalimbali.
“Nchi yetu ilikuwa katika mchakato wa uandikaji wa Katiba Inayopendekezwa kazi ambayo ilikamilika Oktoba 8, mwaka huu.
kazi iliyombele yenu ni kuisoma Katiba hii sura kwa sura ibara kwa ibara.
"Tusikubali kusomewa na tutakapokamilisha kazi ya kuisoma tuipigie kura ya ndiyo,” alisema Dkt. Migiro.
Akizungumza na katika mkutano wa mabalozi wanazoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Watu wa China uliofanyika kwenye Nyumba ya kufikia Wageni ya Serikali ya Diaoyutai, Beijing, Rais wa Jakaya Kikwete alisema Kura ya Maoni inatarajiwa kupigwa wakati wowote Aprili mwaka ujao kama mambo yataenda vizuri.
Rais Kikwete alikabidhiwa Katiba hiyo hivi karibuni mjini Dodoma baada ya Bunge Maalum la Katiba kumalizia kaze yake.
No comments:
Post a Comment